Monday, 9 September 2013

Daz Baba Kwishey

MASKINI Daz Baba! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari ya kusikitisha ya msanii huyo ambaye jina lake kamili ni David Jacob kunaswa akiwa amezima mjini hapa huku ulevi wa kupindukia ukidaiwa kuwa chanzo. Daz Baba au Daz Mwalimu asubuhi ya Agosti 5, mwaka huu alinaswa na kamera za gazeti hili akiwa hajitambui kwenye eneo maarufu kwa jina la Itigi lililopo nje ya Stendi ya Mabasi ya Msamvu ikidaiwa kuwa alifika mitaa hiyo tangu usiku wa jana yake.
Awali chanzo chetu cha habari kilitupigia simu na kutueleza juu ya kuzimika kwa msanii huyo aliyekuwa akiunda Kundi la Daz Nundaz Family na baada ya paparazi wetu kufika eneo la tukio ambalo ni maarufu kwa biashara haramu ya ukahaba, lilibaini kuwa ni yeye na wasamaria wema walikuwa wakijaribu kumuamsha bila mafanikio.
“Huyu atakuwa amelewa sana na inawezekana katumia madawa ya kulevya au kawekewa madawa kwenye bia. Dah! Inasikitisha sana kwa msanii kama huyu ambaye huko nyuma alikuwa aking’ara kwenye anga la muziki,” alisikika akisema kijana mmoja aliyekuwa eneo hilo.
Hata hivyo, jitihada za kumuamsha ziligonga ukuta na mpaka paparazi wetu anaondoka eneo la tukio bado msanii huyo alikuwa hajitambui na mfukoni hakuwa na kitu, ikiashiria kuwa wahuni walimkomba kila kitu.

Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • UJIO WA OBAMA KUFURU UJIO wa Rais wa Marekani, Barack Obama ni kufuru tupu, kiasi cha fedha ambacho kinachotumika kugharamia ziara yake peke yake kinazidi mara mbili ya kile kilichoteketea pale mtangulizi wake, George W. Bush, alipotembelea n… Read More
  • Shilole kaiba simu za Diamond? TAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.Msanii huyo alikumbwa na kas… Read More
  • Mimba ya Penny yatoka? TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa. Kwa mujibu wa chanzo makini kili… Read More
  • Binti alizikwa 2010 aibuliwa Binti Nuru Omari aliyeibuliwa. BINTI aitwaye Nuru Omari anayedaiwa kufariki dunia mwaka 2010 ameibuliwa hivi karibuni wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani na mganga akiwa hai kwenye banda kuukuu. Tukio hilo limetokea kw… Read More
  • Mtaa wa ngono wafumuliwa.... NI hakika ‘mtaa wa ngono’ umefumuliwa! Sakata hilo lilijiri saa tisa usiku, Ijumaa iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori jijini Dar eneo ambalo makahaba wameligeuza chumbani, Operesheni Fichua M… Read More

0 maoni: