Friday 26 July 2013

Kuna ukweli wowote katika hili? Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA!

Asante kwa kuamua kusoma peji hii. Naamini utajadili hoja ukiwa na fikra huru na c utumwa wa fikra. Natambua mchango mkubwa wa mbowe katika kuijenga Chadema. Amefanikisha mipango mingi mizuri kama kuanzisha kanda, M4c na kuongeza wanachama. Pia kajitahidi sana kutatua migogoro mingi ya ndani bila kufukuza mtu. Kwa ujumla C mtu wa Visasi na anabusara kubwa sana juu ya uongozi.

Kwa sasa kwa heshima ya Mbowe naomba aandae utaratibu wa kumkabithi chama Kamanda mwingine anayeaminika uwenyekiti lakini asiwe Dr Slaa au Zitto.

SABABU ZA KUACHIA UONGOZI.;-
Uongozi mzuri ni kuacha madaraka Kistaarabu tena ukiwa bado unapendwa na unanguvu na kubaki kama mshauri.

2. Kuondoa dhana ya kung'ang'ania madaraka ndani ya Chadema.
3. Mbio nzuri ni za kupokezana vijiti ili atakaepokea aongeze kasi, mbinu na ari kufikia mabadiliko ya kweli.
4. Inaweza kupunguza propaganda kadhaa zidi ya Chadema
5. Tuweke tofauti kidogo na wapinzani kwa kukabidhiana madaraka bila kupinduana na kutokuwa na wafalme katika vyama kama ilivyo kwa NCCR, TLP, CUF NA UDP. Na ndio sifa ya Chadema toka awali. Alianza Mtei akaja Makani na Sasa mbowe tena kwa makabidhiano ya Amani

Kiongozi mpya awe na sifa zifuatazo
1. Awe Mwanaharakati na amedhamilia Kuikomboa Tz. Apimwe kwa alivyofanikiwa kuidhiti CCM jimboni kwake ata uchaguzi ukirudiwa leo CCM wasiambue kiti cha udiwani ata kimoja kwenye jimbo hilo. Kama ilivyokuwa kwa Wangwe na sasa Arusha. Hai kuwa na madiwani wengi wa CCM ni dosari kubwa sana kwa Mbowe

2. Awe na uvumilivu mkubwa sana wa kisiasa hasa za ndani ya CHADEMA ASIWE NA HASIRA AU KISASI AU MTAZAMO HASI KWA WATU WANAOTOFAUTIANA MITAZAMO. Hapa Mbowe alifanikiwa sana. Ila Zitto, Lema, Slaa, Lissu labda wafundwe sana ndipo wafikie sifa hii

3. Asiwe na maslahi binafsi Muwazi na mkweli na mwenendo usiotia mashaka.

CHADEMA LAZIMA ITAWALE MEDIA ZOTTE KWA NGUVU ZA MICHANGO YA UMMA KAMA MATANGAZO YA SERA ZAO kwenye magazeti, mikutano yao ya kitaifa kuwekwa laivu kwenye TV NA REDIO VIPEPERUSHI NA CD. Si kilamtu anaYEkwenda kwenye mikutano ya hadhara na haya mabomu yanavyorushwa HIVISASA.

Kitu nachojua MBOWE HAWEZI kukubali Chadema ijitangaze kwenye media au kumiliki media zake yani Redio, Tv stesheni na Gazeti kwani KUKIFANYA hivyo ni kuua soko la Media Zake na anachofanya ni kulinda Soko la Magazeti yake na Redio yake binafsi alizonazo Zinazouza habari za CHADEMA ZAIDI.

Nachochujua Chadema ilichobakiza hadi kuchukua nchi ni kumiki media zake tu. Hatua ambayo mbowe hawezi na baadhi ya wanamageuzi wenyefikira huru huweza kumuhisi kuwa ni Pandikizi na labda kaishakula vya watu na lengo lake sasa ni kuidumaza chadema. Yani ilipofikia ndipo hapohapo na hii kumkamatakamata ni kama maigizo tu ndani ya democrasia yetu. Kwani naona kama amepoooza


Kwa hisani ya Mdau - Uncle W.M

0 maoni: