Monday, 29 July 2013

Diamond awekeza kwenye ardhi?

WAKATI Wema Isaac Sepetu akiongeza idadi ya magari kwa kununua mkoko wa maana, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemziba mdomo baada ya kununua eneo kubwa ambalo ndani yake kuna nyumba tatu, jirani na anapoishi Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Ijumaa Wikienda lina maelezo kamili.Tukio hilo lilijiri hivi karibuni Mtaa wa Kaprikoni-Kijitonyama jijini Dar na kusababisha watu kupigwa na butwaa na kudai kuwa kweli ‘dogo’ ana jeuri ya fedha kwa kitendo hicho cha kununua karibia mtaa wote huo.
Akizungumza na gazeti, hili muda mfupi  baada ya kukamilisha kila kitu kuhusiana na ununuzi wa eneo hilo ambalo kwa mujibu wake anatarajia kujenga jengo lenye ghorofa nne na nyumba za kawaida tatu, Diamond alisema kuwa anajitahidi kuongeza idadi ya mijengo anayomiliki kwa kuwa ndicho kitu cha thamani kuliko magari.
“Najua (nyumba) zitanisaidia endapo muziki wangu utakosa soko. Mimi na mama yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) tuliishi kwa dhiki sana na sasa kwa kipindi hiki ambacho Mungu ananisaidia na kuniwezesha kupata fedha kwa wingi, siwezi kuishi maisha ya anasa ya kununua magari ya kifahari,” alisema.
Katika hali iliyotafsiriwa kuwa ni kumtunishia msuli Wema, jamaa alitupia maneno: “Mimi siyo kama hao wanaokimbilia kununua magari ya kifahari ili mradi waonekane wako juu kifedha. Eneo alilonunua Diamond anayemiliki nyumba zaidi ya tano Dar lipo mtaa wa nne kutoka anapoishi Wema.

Kwa hisani ya Shakoor Jongo/GPL

0 maoni: