Saturday, 6 April 2013

Machangu Wazitikisa Ndoa za WABUNGE

Ndoa za baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinadaiwa kuwaka moto kufuatia kuibuka kwa wimbi la madadapoa raia wa Rwanda ambao wamekiri kuwapa uroda waheshimiwa hao wanapokuwa mjengoni, Dodoma, Ijumaa limeinyaka.

Uchunguzi wa gazeti hili umenasa data kuwa, wake wa waheshimiwa hao walipata mshtuko mkubwa hivi karibuni kufuatia taarifa ya kukamatwa kwa machangudoa hao, Esperance Hagenimana (28), Vestina Zaninika (27) na Ziada Mukamurera (25) huku wawili kati yao wakikutwa na dawa za kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (ARVs).

CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina, taarifa za kukamatwa kwa machangu hao ziliwafanya baadhi ya wake hao wa wabunge kuwa na mashaka makubwa juu ya maambukizi ya VVU kutokana na ‘wauza sukari’ kukutwa na dawa hizo.
“Kwa kweli ndoa zao zimetikisika sana, wake wa wabunge wamepandwa na presha, wamekosa amani, wanahofia na wao wameambukizwa kwani ni dhahiri machangu hao wamekuwa wakionekana Dodoma kipindi cha Bunge au Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),” kilisema chanzo chetu.


MAMA WA MHESHIMIWA
Mmoja wa wake wa waheshimiwa aliyezungumza na Ijumaa kwa sharti la kutotajwa gazetini alisema kuwa dawa sasa hivi hakuna kuwaacha waume zao waende wenyewe mjengoni bali ni kuambatana nao kwani hali si shwari.
 Taarifa zaidi zilidai kuwa, machangu hao waliokuwa wakiishi katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo maeneo ya Area D, mjini Dodoma, wamekuwa wakifanya biashara hiyo katika klabu za usiku ambazo waheshimiwa nao huingia kujirusha.

WABUNGE WANASEMAJE?
Akizungumzia wimbi hilo la machangu mjengoni, Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu (CCM), alisema yeye haliwezi kumgusa kwa sababu si mtu wa kujirusha.
“Mimi siyo mtu wa viwanja, ningekuwa nakwenda hapo sawa, ningeweza kuwazungumzia. Waulizwe wanaokwenda kujirusha,” alisema.
Naye Mbunge wa Mbinga, John Komba (CCM) alisema: “Dodoma nina nyumba yangu, sikaagi hotelini mimi wakati wa bunge. Sasa hao machangu nitakutana nao wapi? Nikitoka bungeni breki ya kwanza ni nyumbani kwangu. Waulizwe wabunge wanaoenda kwenye kumbi za starehe.” 

TAMKO LA BUNGE
Kuhusiana na madai hayo ya maambukizi ya VVU kwa waheshimiwa, Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge, John Joel aliliambia Ijumaa kuwa wabunge wote wanatambua namna ya kujikinga na maradhi hayo na wana kitengo maalum kinachoshughulikia utoaji wa elimu ya maambukizi ya ugonjwa huo hivyo si rahisi kuambukizwa.


Kwa hisani ya - GLP

0 maoni: