Friday 19 April 2013

Maalumu kwa wenye tabia hizi ...

WADADA
Pamoja na kwamba siku hizi nguo za ndani kama braa na chupi zimejaa kariakoo, mchina alisharahisisha huduma kwa bei chee tu ya 1000 ushapata cotton yako japo ya low quality BADO inashangaza unakuta mdada mrembo kweli kweli, high hill zake, kiswanglish kwa sana tu na mapozi kibao anavaa chu***pi hadi inaota sugu za uchafu maeneo flani.. kwenye hanger amejaza mich*upi myeusi na hata zikiwepo nyeupe basi zimefubaa hadi aibu......(hii siongei bla bla nimeona kwa macho yangu kwa baadhi ya wadada tena wenye elimu zao (master na bachelor) na kazi zao za maana tu, ofisini wanaheshimika kweli kumbe usafi kwao 0)
........kwanza nani alikuambia ch*u*pi ya mwanamke ni nyeusi?? labda kwa mida flani tu unaweza kuwa na black lakini mwanamke shuti usafi na rangi nyeupe au pink ndio rangi za kike, rangi hizi ni kipimo halisi cha namna ulivyo msafi. Unakuta kinguo cha ndani kimevaliwa miaka nenda rudi hata hakibadilishwi?? Kwani hukufunzwa ulipokuwa mtu mzima (i.e. baada ya kuvunja kikombe) ?? 

Haya tena, utakuta kibraaa nacho kimechinaaaa utadhani kimefukizwa moshi na mvaaji ni mpishi wa mashuleni. Jitahidini walau, huduma zimerahisishwa na mchina siku hizi. Usafi sio foundation usoni na wanja....

WAKAKA
 Unakuta mkaka handsome kweli kweli, amechomekea design, upanga wa surual ya kushona ndo usiseme....mdada unaona hapa nimepata wa ukweli. Sasa siku ya siku unamkaribisha kwako, mgeni shuti kuvua kiatu mlangoni, harufu inayotema hapo hata mood yote inaisha. Kumwambia huwezi, basi na yeye ndo amekazia kweli kuleta story zake as if ile harufu yeye haijaingia kwa pua zake. Unakuta socks inavaliwa wiki nzima na mijoto ya dar utadhani madukani zimeisha...... nunua pea hata 30 walau kila siku na socks zake, pia jaribu kuweka viatu vyako kwenye jua angalau kila wiki mara moja au mbili wakati wa week end. Kama unanuka miguu sababu ya ugonjwa basi jaribu kwenda hospitali mapema utibiwe. Wajameni eeh tujikague na kuweza kutambua harufu hizi ili zifanyiwe kazi mapema isiwe kero. Hata poda ya 500 tu ukiwa unaipaka miguuni ndio uvae socks then viatu inakata harufu yoote ya miguuni. 

Na boxer zenu za kijani, brown na njano.....mhh sijui wengi wenu hamzifui? mkaka akivua tu nguo harufu hiyoooo mhhh kwakweli mnakatisha tamaa sana. mfano mzuri ni kule mabibo hostel ukiingia tu kwenye vyumba vya wakaka walio wengi (sio wote msije niparua) utakuta kunatema harufu flani kama mixer ya janaba na uvundo hivi. Najua wengi mtabisha ila ndo hivyo mie nshatoa yangu. 

Hii ni kwa wanaume walio wengi wakubwa kwa wadogo. Mwanaume utabaki kujiuliza mbona mie kila nikitongoza sikubaliwi....kumbe mwenzako alichoka na hali kama hizo na hivyo mood yote ya kukukubali imemtoka. Ni jambo dogo ila lina madhara makubwa.

0 maoni: