Wednesday, 20 February 2013

Ndoa hupangwa na MUNGU! Mama yake Monalisa (NATASHA) achumbiwa.....

LICHA ya kuwa mtu mzima mwenye mtoto na wajukuu wawili, staa wa filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ amechumbiwa. Habari za uhakika kutoka katika chanzo chetu makini zinasema kwamba, Natasha alivalishwa pete ya uchumba wikiendi iliyopita, Yombo – Dovya, Dar na mwanaume anayetambuliwa kwa jina Alex Humba Ludamila.

“Ilikuwa hafla ya siri kubwa, Natasha hakutaka kabisa waandishi wa habari na kwakweli siwezi kukutajia eneo lakini fahamu kwamba ni Yombo – Dovya. Unajua huyu ni mwanaume wake wa muda mrefu na walikuwa wakiishi pamoja lakini jamaa kaamua kuchukua jumla ndiyo maana amefuata taratibu zote,” kilieleza chanzo hicho.
Pekupeku za Tollywood Newz zilinasa kuwa, kwa sasa mipango ya ndoa imepamba moto na ndoa inatarajiwa kufungwa mapema mwezi Mei, mwaka huu. Juhudi za kumpata Natasha ili azungumzie suala hilo ziligonga mwamba baada ya simu yake kutopatikana muda wote Jumapili na juzi Jumatatu alipopigiwa.

Kwa hisani ya GLP

0 maoni: