People's Magazine
The place where you can find everything...
Home
Wednesday, 27 February 2013
Home
»
Celebrities News
» JOSEPH SHALUWA amchana live JACK wa CHUZ
JOSEPH SHALUWA amchana live JACK wa CHUZ
By
Unknown
14:05
No comments
Kwako,
Jacqueline Pentizel ‘Jack wa Chuz’. Pole kwa changamoto ulizokutana nazo juzi hotelini wakati ukiwa na mteja aliyetaka kuspendi na wewe kwa dola 500. Ni ajali kazini, usiwaze sana.
Tatizo nini ujue sister? Unawadanganya watu. Unapindisha ukweli kuwa uongo. Hapo ndipo ulipokosea zaidi. Siku zote binadamu anapokuwa mkweli ndipo anakuwa huru.
Kudanganya wakati mwingine kunaweza kuwa na maana kama unaongopa kwa lengo la kuficha kitu chenye manufaa lakini pia uwe na ushahidi au mazingira ambayo unaowadanganya hawatakushtukia.
Ni kweli wewe ni muongo, tena muongo mkubwa mwenye ‘shahada ya kwanza ya uongo’ uliyoipata katika Visiwa vya Madagascar ila sasa inaonekana huko ‘chuoni’ ama ulikuwa unachungulia majibu au ulikuwa unatoka na profesa akawa anakubeba!
Gazeti hili toleo lililopita liliripoti habari ya kukunasa ukiwa kwenye mtego wa kwenda kuuzwa kwa ajili ya kufanya ngono kwa dola 500. Siyo siri, muuazaji mwenyewe ni Baby Candy na anaujua ukweli huu, kuwa alikuwa kazini kukuuza. Ushahidi wa kutosha upo.
Kama chombo cha habari siku zote tuko macho kumulika maovu yanayofanywa kwenye jamii. Tukiwa katika kutimiza majukumu hayo hata siku moja hatumsingizii mtu. Tunasimama katika ukweli.
Tunajua ukweli unauma na wengi hawapendi kuambiwa ukweli, wewe ni kati ya watu hao. Mbaya zaidi wakati ukikanusha kwenye runinga unajua wazi kuwa tukio ni la kweli na si filamu kama ulivyokuwa ukijaribu kudanganya.
Nidhamu na maadili unapaswa kusimamia mwenyewe, ukiteleza na kunaswa usitumie nguvu kukanusha, kuwa mkweli. Yaani umenaswa ukitaka kuingia mzigoni na mapatano yamefanyika tena kila kitu kimerekodiwa, gazeti linatoka asubuhi jioni yake tayari upo kwenye kituo cha runinga unakanusha!
Hebu kuwa mkweli mtoto wa kike, kuna filamu ya aina ile? Wasomaji wa Global kwa namna walivyo makini na wakomavu hawawezi kukubaliana na upuuzi uliouongea kwenye runinga. Wanajua unatapatapa tu!
Eti unasema ulikuwa unarekodi filamu?! Ipi? Prodyuza ni nani na mhusika mkuu ni yupi sasa pale? Acha uongo wa kitoto. Ili usiandikwe ishi kwa staha. Wewe ni mtu maarufu, watu wanajifunza kupitia maisha yako, utawaponza hata wasanii wengine chipukizi wenye nia ya kuingia kwenye soko la filamu wazuiwe na wazazi wao wakiamini lipo soko jingine nyuma ya filamu.
Kuishi kwa kutegemea biashara haramu hakuna maana, umepewa kipaji cha sanaa, kwa nini usikitumie vizuri kutafuta riziki yako badala ya kutafuta shotikati?
Acha uongo wa kizamani. Nakuasa usitumie mwavuli wa sanaa kufanya mambo machafu yasiyokubalika katika jamii ya kistaarabu ya Kitanzania.
Utakuwa muungwana kama ukirudi tena kwenye jamii yako na kuitaka radhi si kukanusha kwa maelezo yasiyo na mbele wala nyuma. Fikisha salamu zangu kwa Baby Candy.
Yuleyule,
Mkweli daima,
Joseph Shaluwa
Kwa hisani ya GLP
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Categories:
Celebrities News
← Newer Post
Older Post →
Home
0 maoni:
Post a Comment
Social Profiles
Popular
Tags
Blog Archives
Search this Blog
Swaga za Lady GAGA...
Angalia picha za BEYONCE ndani ya H&M campaign
Hii ni hamu au ugonjwa? ........ nisaidieni
Jamani mimi na mpenzi wangu tupo pamoja kama mwaka na nusu sasa, na tumeanza kufanya ngono kama miezi nane hivi lakini cha ajabu mwen...
Chezea Jeshi wewe!
Dhahama hii iliwapata hawa wakaka baada ya kukatika kwenye eneo la jeshi.................. mmmmmh jamani wanastahiri adhabu hii? Je kulikuwa...
'White Widow' plotted to blow up UN offices and Western embassies ahead of Nairobi mall attack
Samantha Lewthwaite was a 'key actor' in plan to attack Western-linked buildings and the Kenyan parliament Intelligence report le...
Ipe maneno hii picha...
Ndani ya Bunge la Tanzania...... Utoro wa wabunge unaonyesha uhalisia wa nafasi zetu kwenye mioyo yao, kwa hali hii utapata picha ha...
Muogope mtu huyu .... Ndie Kiongozi wa kundi la Wezi wa Power Window Tanzania, Rama Jangiri…
Huyu ndiyo kiongozi wa kundi la wezi wa power window Tanzania, Rama Jangiri…Hapa ni baada ya kukamatwa huko tegeta akiwa hotelini ...Alikama...
Shine like a star... Serena Williams poses up a storm as she shows off her winning figure in monochrome bikini
Aibu! babu Anaswa gesti akila uroda na denti Wa Sekondari huko Maeneo ya kawe jijini Dar
OMG.... Wastara ni mzuri jamani hebu angalia piza hizi
Powered by
Blogger
.
My favorite News blog
Loading...
Celebrities Gossip
Loading...
.
Tags
Afya
(116)
Broken heart stories
(1)
Celebrities kids
(18)
Celebrities News
(783)
Children
(4)
Death Anouncement
(1)
Dini
(27)
Elimu
(5)
Extraordinary People
(12)
Familia
(26)
Full aibu
(87)
General
(20)
Karibu Jamvini
(1)
Katuni
(11)
Kazi za Jamii
(3)
Magazeti pendwa
(228)
Mahusiano
(281)
Majanga
(16)
mambo ya kuiga
(3)
Mapishi
(2)
Michezo na Burudani
(49)
Mikasa ya Maisha
(2)
Mila na desturi
(14)
Moyo Mpweke
(3)
Msaada kwenye tuta...
(10)
Nyumba
(28)
OMG
(476)
OMG... Black are beautiful
(10)
Picha huongea
(25)
Sayanzi na Tekinolojia
(3)
Siasa
(82)
Tangazo
(2)
Tiba Mbadala
(4)
True story
(77)
Ugaidi
(1)
Ukatili
(55)
umaarufu kazi
(28)
Urembo
(20)
Video
(10)
Vipaji
(3)
Vituko mtaani
(164)
Vivazi na Mitindo
(171)
Wanaume
(32)
Wanawake
(121)
0 maoni:
Post a Comment