Friday 25 January 2013

Baada ya Wema, Jokate, Avril sasa ni zamu ya Penny wa DTV? Diamond kiboko


Diamond Platinum ataendelea kuuza magazeti ya bongo kila siku na hii inatokana na vituko anavyoibuka navyo kila siku! Hauwezi kupita mwezi bila kuibuka kitu kitakachomfanya aandikwe tena na tena.
Katika picha iliyowekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa msichana aitwaye Skyner Ally kuna picha inayomuonesha Diamond akiwa amelala kimahaba na msichana anayedaiwa kuwa ni mtangazaji wa DTV, Penny Mungilwa aka Vj Penny.
Hata hivyo tulipowasiliana na Penny alisema hiyo ni picha iliyopigwa walipokuwa kwenye scene ya movie wanayoigiza pamoja ambayo amesema hana uhakika lini itatoka! 

Penny na Diamond  ndani ya  movie?????...!!? Ngoja  tuisubiri tuione hiyo movie


0 maoni: