Wednesday, 5 December 2012

Baada ya Maisha kumgonga Mwinyi ampigia Magoti Jay dee

Ama kweli ujanja mwingi mbele giza.......... na ile methali inayosema  usitukane wakunga na uzazi ungalipo imeanza kufanya kazi katika maisha ya Mwanamuziki wa zamani wa Machozi Band , aliyefahamika kwa jina la  Mwinyi Goha (pichani akiwa na flowers enzi za machozi). Inasemekana hivi karibuni Mwinyi  kampigia magoti Lady Jay dee eti kisa amrudishe kumbini! lakini wambea wamji wametujuza na kusema Mwinyi aliondoka vibaya tena kwa kashfa na maneno tele  huku akidai amechoshwa na uongozi wa kibabe, wenye dharau na ubabaishaji wa Lady Jay deee, hakuishia hapo Mwinyi pia alisema  Jaydee ana roho mbaya , anamlipa hela ndogo tena inatoka kwa maneno kibao...........  

Habari zilizotufikia  toka kwa wambea wa mji wanasema eti Lady Jay Dee kupitia ukurasa wake wa Facebook amedai kuombwa radhi na Mwinyi na  kutaka   arejeshwe kundini........ 



“Nadhani wote mnamkumbuka Mwinyigoha, aliekuwa MACHOZI BAND kitambo. Baada ya yote yaliotokea na mlioyasikia anataka kurudishwa kundini, Naomba mvae kiatu changu…, Je ingekuwa wewe ni JIDE ungemsamehe na kumrudisha tena kazini?? Jiweke kwenye nafasi yangu unipe jibu,” ameandika Jide.


Ila sasa hapa sijui Jide anaomba ushauri kwa mashabiki wa machozi Band kiukweli au ndio anataka kumdhalilisha  Mwenzake tu ? mmmmm na Washabiki wakimshauri Kumrudisha Mwinyi je atakubali kuufanyia kazi ushauri huo? yetu macho na masikio tunasubiri.......

0 maoni: