Friday, 15 August 2014

Mkono wa rubani wang'oka hewani


Rubani mmoja nchini Uingereza alipoteza mwelekeo angani akiendesha ndege ya biria baada ya mkono wake wa bandia kuchomoka wakati alipokua akielekea kutua.
Rubani huyo wa shirika la ndege la Flybe mwenye umri wa miaka 46 , aliruka kutoka uwanja wa ndege wa Birmingham, akiwa na abiria wapatao 47 ndani yake, wakati alipokaribia kutua katika uwanja wa ndege wa mji wa Belfast alikumbana na upepo mkali angani ambao ulimsababisha atue kwa ghafla ilivyo bahati hakukuwa na madhara kwa ndege yenyewe wala abiria.

Katika maelezo aliyoyatoa baada ya manusura, mkurugenzi wa shirika hilo la ndege la Flybe Captain Ian Baston, anayehusika pia na masuala ya usalama katika shirika hilo la Flybe alimuelezea rubani kiongozi wa ndege hiyo aliyekua akiiongoza kuwa ni mwenye uzoefu wa hali ya juu na mwenye kuaminiwa pindi awapo angani, na hivyo usalama wa abiria na wahudumu huwa katika mikono iliyo salama sana .

Muda mfupi tu kabla ya kuielekeza ndege Dash 8 kutua kwa dharula rubani huyo alijikagua na kuona kwamba mkono wake bandia wa shoto ulikua sawa lakini baada ya tukio hilo ghafla akajikuta mkono huo umechomoka.

Ndege hiyo ilitua kwa mlio mkubwa ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa na pia ndege haikuharibika.

Rubani alisema atakuwa makini zaidi katika siku za usoni kuhusiana na mkono wake huo bandia.

Kwa hisani ya BBC Swahili

0 maoni: