Sunday 16 February 2014

Kuna ukweli wowote katika hili? Lema akamatwe na kushitakiwa kwa kosa la UHAINI!


Ndugu zanguni,

Nimekuwa nikifuatilia kwa makini kauli na vitendo vya kichochezi vinavyofanywa na Mbunge wa Arusha Mheshimiwa Lema na nimeridhika kabisa kuwa Lema ni mhaini ambaye inabidi akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuchochea machafuko nchini. Lema alisema Rais amepandikiza udini nchini na ushahidi anao. Lema alitengeneza sms kwenye internet kuonyesha mkuu wa mkoa wa zamani wa Arusha kamtishia
Mikutano yote ya Lema huwa ana watukana viongozi wa nchi na kuwashinikiza watu wafanye vurugu na pia kuchochea uvunjifu wa amani, 

Lema leo anadai Rais kawaagiza polisi kuua na vijana wa ccm kupiga wapinzani.

Huyu mtu ambaye ni kiongozi wa wananchi, akiachwa aendelee na huu mdomo wake mkubwa bila kudhibitiwa ni hatari kwa usalama wa taifa.

Lema ametenda kosa la uhaini na ni lazima afikishwe mahakamani, laa sivyo tutegemee wenzake kuiga na kueneza chuki kila kona ya nchi jambo ambalo ni hatari sana kwa usalama wa taifa.

Lema anafanya hivyo kwa makusudi kabisa kwa sababu ndio njia pekee ya kujipatia umaarufu kwa viongozi wa chadema

Ukiona swala anachezea sharubu za simba ujue anataka kuliwa....

Polisi wakiendelea kumchekea Lema watakuwa wanahatarisha amani ya nchi.


0 maoni: