Wednesday 13 February 2013

Wanaume wenye sura hii, wana misimamo ambayo hawako tayari kuivunja…!

Watu wenye sura hiyo hapo juu naamini kila mmoja wetu anaweza kabisa kuwa anamjua angalau mtu mmoja mwenye sura inayofanana na hiyo. Watu wenye sura hiyo ni watu ambao wana sifa ya uzungumzaji, usafi na wakati mwingine ukorofi na hasira zilizojificha. Ni watu ambao huzungumza sana na hasa kama masuala husika wanayajua au kuyapenda. Kwa hiyo kama ni kwenye siasa, mpira, dini au kingine ambacho wanakifahamu kwa kiasi fulani, huwa ni wazungumzaji sana.
Watu wenye sura hiyo ambao ni wachafu sio wengi, kwani kwa sehemu kubwa huwa wanajipenda katika kuvaa na kuoga, yaani usafi wa miili yao. Siyo jambo la ajabu kukutana na mwanaume mwenye sura hiyo ambaye hana hata senti kumi, lakini akiwa amevaa vizuri na ni msafi sana.


Wanaume wenye sura hiyo kama wanakunywa pombe au kuvuta bangi, hawana amana kwani hutokea kuwa wakorofi. Kama wanapenda wanawake pia hutokea kunaswa kirahisi na kwenda hovyo. Lakini wana sifa moja, ambayo ni uangalifu. Hata kama watakuwa kwenye tabia fulani mbaya, hujificha sana na kuwafuma huchukua muda.

Kwa kawaida wanaume wenye sura kama hiyo siyo wazungumzaji sana. Ni wapole, hasa pale ambapo wanajua wakisema sana, kutazuka kelele au kusigishana na pengine huogopa kukosolewa. Lakini nje ya kuhofia kusigishana huwa wasemaji wazuri, wanaopenda kusikilizwa wao tu. Kwa hiyo, kwa asili ni wapole, lakini kwenye mazingira fulani, ni wazungumzaji sana.

Wanaume wenye sura hiyo wana hasira za chini chini au tuseme, hukasirika haraka lakini huficha kwanza. Kwa hiyo badala ya kusema hunyamaza, lakini huumia ndani kwa ndani. Hii mara nyingi sana huwaumiza kihisia na baadaye kimwili, ambapo hupata maradhi kama ya moyo, kisukari , shinikizo la damu na mengine.

Wanaume wenye sura hiyo hufuata sana kanuni na taratibu zilizowekwa na jamii na hutokea kuwa waaminifu kwa kazi au mali za watu. Kuna idadi kubwa ya wanaume wenye sura kama hiyo ambao ni waaminifu sana. Hufanya kazi kama yao wanapoaminiwa na kupewa uhuru wa kufanya. Wanapenda kulinda majina na heshima zao hata kama kwa kufanya hivyo hawapewi shukurani.

Kwa upande wa ndoa au mahusiano hawana matatizo sana na kinachowasaidia ni misimamo yao. Wanaume wenye sura hiyo wana misimamo ambayo hawako tayari kuivunja, iwe ya kazini kwao au kwenye ndoa zao. Lakini pia mara nyingi ni watu wanaopenda kubaki na wake zao wa awali, hata kama wanatokea kuoa tena. Lakini hata hivyo,tabia ya kuwa na wake zaidi ya mmoja au nyumba ndogo, haiwakumbi sana wanaume wenye sura kama hiyo.

Kwa kawaida hupata bahati ya kuoa wanawake ambao ni wachapa kazi, wakomavu na wenye juhudi. Lakini wake zao wanapobadilika kitabia huwa wasumbufu sana. Hata hivyo hawatoi nafasi kwa wake zao kubadilika kutokana na misimamo yao. 

Kwa kawaida wanaume wenye sura hiyo ni watu wa kipato cha kati, elimu ya kati na umaarufu wa kati. Hawapandi juu sana na wala hawashuki sana. Pamoja na hayo yote, hujitahidi kufahamu vitu vingi au kupenda kujifunza kupitia kwa wengine.


Mdau - Mtambuzi

0 maoni: