Friday 8 November 2013

Kuna ukweli wowote katika hili? Naonekana sina faida ndani ya CHADEMA, nimeng'oka rasmi kuanzia leo

Ndugu wana.JF


Juzi niliweka uzi hapa na nikatoa mda wa masaa 24 kwa Mh Mbowe na Dr.W.Slaa kusema neno juu ya hali ya siasa iliyokuwepo chadema, specifically kwenye issue ya Viongozi wawili..Lema na Zitto kulumbana mtandaoni. Katika hali iliyowazi, niliona mwendelezo wa siasa nyepesi na za kijinga kabisa kutoka kwa Mh.Lema za kutaka kujinasibu kuwa yeye ni mfia chama na anapambana na wanafiki wakati wapo ambao tayari wamepoteza maisha wakiitumikia chadema.
Siku zote nimekitumikia chadema, kwa Rasilimali fedha, mawazo na hata kazi kubwa ya kupunguza kasi ya mashambulizi kutoka kwa CCM kwenye mitandao. Wakati wote nimekishauri chadema kuhusu umuhimu wa kuimarisha mfumo wa kiuongozi ili kuondokana na miungu watu ndani ya chama, nliwahi kukutana na John Mrema nkamshauri umuhimu wa kuimarisha Baraza la wanawake chadema kwa maana ya kwamba "tukiweza kupata trust from women, tumeipata jamii yote". Nimeshauri umuhimu wa Chadema kuwa na chombo chake cha habari, tofauti na sasa ilivyo chadema inategemea Tanzania Daima gazeti ambalo mmiliki wake ni mbowe. Kati ya yote hayo hakuna ushauri uliofuatwa wala hata ku acknowledge. NIMEONEKANA SINA FAIDA CDM.

Ndani ya chadema kuhoji jambo ni kugusa maslahi ya viongozi, kusema kwamba Mbowe kakiuzia chadema magari chakavu, unavuliwa uanachama. Mtu ukisema una nia ya kugombea nafasi katika chama, kinatumwa kikundi kinachoratibiwa kwa umakini sana na Josephine Mshumbusi kuchafua watu katika mitandao.

Chadema sasaivi wameshindwa kufuata misingi thabiti ya chama, na imebakia na miungu watu, haingii akilini DR W Slaa anakuja hapa Jamii Forums anaanza ku-LIKE post na comments za watu wanaomponda Zitto Kabwe, ni nini tafsiri yake? Katika hili ukisema sio vizuri, unatukanwa na kukanywa kuingilia chama, na nimetumwa.

Tumepigana sana kuijenga chadema mitandaoni, sio kwa ajili ya kutetea watu kama baadhi ya makamanda walivyo biased ila chochote tulikitetea ilimradi tu ni kwa ajili ya chama..lakini hizi juhudi zetu haziwi acknowledged.

MAAMUZI YANGU 
--------------------------------------------------
LEO tarehe 7 november 2013 ninang'atuka chadema hiki chama sii mamaangu. Nachukuwa maamuzi haya kama alama ya kuwajibika, na kujiondoa katika mnyororo wa ujinga uliopo chadema. Ni aibu kwa kijana kama mimi kuwa sehemu ya ujinga na unafiki, siwezi kukubali kuburuzwa na wanaojidai wanasiasa.

Tayari list ya makada maarufu wamefikia azma ya kujitoa chadema na kwanzia leo tutege masikio yetu . Mimi nimewahi kwa sababu niliahidi after 24hrs ningekuja na maamuzi magumu. Makamanda nimewasihi kuwa na maamuzi yao binafsi, nisiwasukume ila wameahidi kugomea kazi ya uenezi wa chama.

Baada ya muda atakuja Kamanda ambae ana utumishi uliotukuka kuja kuorodhesha maswala 24 ambayo kama makada watayagomea ndani ya kamati kuu na chama, wao wameahidi hawatajitoa.

Tanzania yangu kwanza, wanasiasa muniache kwanzia sasa.


Ka hisani ya - JF

0 maoni: