Friday 11 October 2013

P- Square kutua Bongo

WASANII wanaounda kundi la P Square, Peter na Paul Okoye wanatarajia kutua nchini kwa ajili ya kutoa burudani Novemba 23 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa na East Africa Radio na TV na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa onyesho hilo, Hillary Daudi kutoka East Africa Radio, alisema onyesho hilo litakuwa la kipekee na litahusisha pia wasanii kutoka Tanzania.

“Wote tunatambua namna kundi hili linavyofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika, licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, pia litatoa fursa kwa wasanii wa ndani kujifunza kutoka kwa wasanii hawa vijana ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi yao ya muziki,” alisema.

0 maoni: