Thursday 31 October 2013

Ndoa ya BOB JUNIOR yavunjika kwa sababu ya huyu dada?

Mwanamuziki mahiri wa Bongo Fleva  anayejulikana kama Bob Junior  (pichani) anadaiwa kuachana na mkewe huku yaliyo nyuma ya pazia yakibaki utata................... 

Bob Junior  mwenyewe kupitia kipindi cha  Power Jams cha East Africa Radio hivi karibuni  alifunguka na kusema  kuwa ameachana na mkewe kwa sababu ya wivu wa Mapenzi , hakuishia hapo alitoa madongo kwa  kwa wale wote  waliozusha kuwa alioa ili aweze kupikiwa futari kipindi cha mfungo .


Ila habari tulizozinyaka kitaa zinasema Bob Junior ni muongo kwa sababu mkewe kashindwa baada ya kijana kuzama kwenye wimbi la mapenzi na msichana  muigizaji wa Kenya anayejulikana kama Ashley Toto(pichani)............

Chanzo kimeendelea kumwaga mchapo na kusema  kuwa wawili hawa wapo mapenzini kwa muda mrefu sana , na hata Bob Junior alipokuwa Ujerumani  alikuwa nae.......... kama baadhi ya picha zinavyoosha wakila maraha.........Pia inasemekana kuwa baada ya Mwanadada huyu kuja  mapumzikoni Mombasa  hivi karibuni  Kijana nae (Bob Junior) alienda huko na Kukaa kwa muda wa week moja  wakiwa  wote ............ na hii  inawezekana ndio sababu mojawapo ya mke Bob Junior kushindwa.........

Nani mkweli nani muongo.......... Stay tune......

 Angalia picha mbalimbali za Bob Junior na Ashley Toto hapa chini





0 maoni: