Tuesday 23 July 2013

Msaada tutani ........Mume wangu kanizidi mshahara lakini kila mara yuko kwenye money crisis

Katika miaka yote tangu tumeoana mume wangu amenizidi kipato kwa maana mshahara wake ni mkubwa kuliko wa kwangu..lakini mara kwa mara yeye analalamika hana pesa. Sio tu kwamba analalamika lkn ukiangalia ni kweli hana na sijui anapeleka wapi.. Matumizi ya nyumbani yote tumegawana almost 50/50 lakini hata hiyo 50% yake tuliyokubaliana anashindwa inabidi nimsaidie . 

Tumefungua biashara nyingi pamoja lkn zote zimekufa kwa sbb yake. Akienda dukani mathalan anachukua pesa anasema atarudisha na harudishi, biashara inakufa kwani anachukua pesa nyingi mtaji unakufa..Nimejitahidi kurudisha mtaji ili biashara zisife akiahidi kutorudia kuchukua tena lkn anarudia mpaka nikachoka nikaacha biashara zikafa.(niliamua kufungua biashara nyingine mwenyewe bila kumshirikisha na inafanya vizuri hadi sasa hajui naogopa nikimwambia tu ataanza kwenda kukopa mwisho ife tena) Anadaiwa na marafiki zake kila siku anawakopa,..huko kazini pia amekopa, na mimi pia ananikopa lkn hata siku moja hajawahi kunirudishia (na mi pia simdai huwa nasamehe tu)

Tumefungua akaunti za wtt ambapo kila mwezi tunakatwa mishahara pesa inaingia huko lkn kuna siku niligundua amechukua pesa zote kwny account za wttPamoja na ratiba tuliyopeana ya kusaidiana anaweza akakaa hata miezi 3 hajatoa chochote nyumbani yaani kama ningekuwa sina kazi sijui ingekuwaje. Kwa kiasi kikubwa mimi ndiye ninayehudumia familia(namshukuru Mungu kazi yangu ina vi-safari vingi vya hapa na pale vimenifanya tuishi vzuri tu) 
Unaeza kufikiri kwamba ana mshahara mdogo lkn ana mshahara mzuri tu, tena analipwa in USD wakati mimi mtumishi wa umma na kijimshahara changu cha kuunga unga na sijawahi kuishiwa na ninafanya mambo mengi kuliko yeye..  Pamoja na kuajiriwa lkn pia ni mtaalamu wa komputa kwa ivo anafanya kazi zake private na anapata pesa nzuri tu nje ya mshahara..

Matatizo yake akiwa na pesa.
1. Siku akiwa na pesa huwa anachelewa sana kurudi nyumbani yaani akiwahi ni saa 4-5 usiku. Huwa anakutana na marafiki baa eti kuongea masuala ya biashara ambako wanazitumbua hizo hela yeye akiwa mfazili mkuu wa meza.

2. Siku pesa zikiisha anawahi sana kurudi nyumbani na anakuwa mpole kupita kiasi na sometimes mkali kupita kiasi(hasa akiombwa hela)

3. Hana na wala hajui kupanga bajeti, akipata pesa anatumia zote..anaishiwa hadi hela ya peroli ya kumpeleka kazini na ht pesa ya lunch akiwa ofcn..

4. Mshahara wake hauchukui zaidi ya wiki umekwisha wote. Hajui kuweka akiba na sijui katika maisha yake km alishawahi kuweka akiba..(mimi nina akiba ya kutosha tu benki nyingine nimeweka huko na kila mwezi napeleka hela) 

5. Hata kama ni kwenye ujenzi anatumia pesa yote huko habaki hata na senti ya kula luch ofcn achilia mbali chakula cha nyumbani..

6. Akipata pesa ananunua chochote atakachokutana nacho hata km hakihitajiki kwa wkt huo..mfano anaweza nunua seat cover za magari yote kwa mpigo na sio kwamba zilizopo zimechoka..au akanunua gari mpya wakati tuna magari ya kutosha tu hapo nyumbani..

7. Nafikiri kila mwezi ananunua simu ya mkononi, wkt mwingine hata simu 2 utaona mpya na mimi ananiletea wakati zangu nzima na nzuri.(Mie huwa sinunuagi kabisa simu kwani chumbani kwangu kuna droo imekaribia kujaa simu na zote nzima) 
Kama anatoa mchango km wa harusi hivi anaweza toa laki 5 mchango ambapo ht angetoa laki 1 ingetosha tu. 
Akiwa hana pesa ni mtu mzuri sana mtapanga mikakati kibao lkn akipata pesa tu hazungumzii tena hiyo mipango yenu..hata ukimkumbusha hataki kuongelea hayo mambo.. anaweza kukurupuka na mipango yake mipya aliyojadiliana na marafiki zake na kuanza kuimplment kwa sapraiz tu..akikwama ndio anakuja kwangu nimsaidie

Mara kwa mara nimemuweka chini na kumueleza matumizi sahihi ya pesa na nimemuomba apange bajeti na aifuate lkn wapi..anakubali akiwa hana pesa akipata tu, anakuwa mtu tofauti kabisa. Nimejaribu kumshirikisha kwenye masuala ya pesa lkn mwenzangu hatoi ushirikiano na hasemi ukweli linapokuja suala la pesa..anaweza akanidanganya kapata kazi ya milioni 5 kumbe kapata 15m au zaidi 
Kuna siku ananipa pesa za matumizi ya nyumbani vzr tu km tulivyokubaliana lkn hata mwezi hauishi anaanza tena kunikopa (actually ni km anazichukua tena zile pesa za matumizi alizonipa)
Uzuri hana tabia ya kuuza vitu hapo nashukuru mana nafikiri angeshauza na nyumba tunayoishi japo tumejenga wote.
YAANI WADAU NISAIDIENI NIFANYEJE? NIMECHOKA MWENZENU NA HII HALI,
Najikuta kila kitu cha familia kuanzia chakula, ada za watoto, nguo n.k nafanya mimi kwa sbb mwenzangu hawezi kumanage pesa zake..N
Mara nyingi na yeye pia namsaidia wakati akiwa kaishiwa mana anaishiwa vibaya, hata hela ya lunch anakosa..
Nimefikia mahali hata mimi mwenyewe nimechoka na yeye hata hajirekebishi

Aunt K

0 maoni: