- Aelezea uhusiano wake na Mwigulu, Lwakatare
- Asema yeye bado ni mwanachama hai wa Chadema, amkwepa Kibanda
SIKU chache baada ya Mahakama kumuachia kwa dhamana mshitakiwa mwenza wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Joseph Ludovick, amefunguka na kuelezea tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, ikiwamo uhusiano wake na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.
Ludovick, ambaye anadaiwa kurubuniwa na Nchemba na hivyo kumrekodi Lwakatare wakipanga mipango ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, alijitokeza juzi katika mtandao wa kijamii wa Mabadiliko na kuomba kuulizwa jambo lolote, kwa kile kilichoonekana kutaka kujibu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake.
Ludovick, ambaye anadaiwa kurubuniwa na Nchemba na hivyo kumrekodi Lwakatare wakipanga mipango ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, alijitokeza juzi katika mtandao wa kijamii wa Mabadiliko na kuomba kuulizwa jambo lolote, kwa kile kilichoonekana kutaka kujibu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake.
Maswali na majibu yake ilikuwa ni kama ifuatavyo;
KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MWIGULU
Akielezea uhusiano wake na Mwigulu baada ya kuulizwa swali na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Dello, Ludovick alisema ni wa kawaida na kwamba haufikii kama ule wa Lwakatare na Maggid Mjengwa.
“Tumejuana kwenye mitandao ya kijamii na tukadevelop ukaribu, ilitokana na mimi kukosoa mijadala yake na kumpinga.
“Ninayo mahusiano na watu wengi tu nje ya Chadema. Mfano ni huyo Mwigullu, Sixtus Mapunda, Mbunge Kangi Lugora, nk.na sidhani kama ni dhambi hii. Wapo wengi tu wenye uhusiano kama huu. Wote hawa katika nyakati tofauti tumesaidiana mengi.
Katika swali lake lingine, Abdul Dello alihoji: “Ludo, Mwigulu Nchemba alithibitika kukutumia m-pesa ya elfu 50 ilikuwa ya kazi gani?
Ludovick alijibu akieleza kuwa: “Nilikuwa na tatizo binafsi la kifamilia, nilihitaji msaada.”
KUHUSISHWA NA USALAMA WA TAIFA
Mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Hamad alimuuliza akisema:
“Ludo, unasemwa sana mtaani kuwa wewe ni TISS Agent (wakala wa usalama wa taifa) uliyepachikwa pale Chadema kwa ajili ya kuiua kifo cha kawaida na ndiyo maana unafanya kazi nyingi za kujitolea badala ya kwenda kufundisha kama taaluma yako ya ualimu inavyokuruhusu, kweli?
Majibu ya Ludovick yalikuwa hivi: “Nchi hii tunapenda majungu tuuu, na magazeti yetu yamebobea kusambaza majungu na kupakazia watu. Huwezi kuelewa dhana hii hadi ikukute. Juu ya kazi ni tofauti za kimtazamo, so wengine wanapenda kuajiriwa na wengine hawapendi, so haicount hii. Ni uamuzi tu. Niliijua Chadema 2006 na kujiunga rasmi 2009. Hakuna aliyenipachika huko. Ni by conviction, nakuhakikishia hata matatizo yote ninayoyapata ni kwa sababu ya Chadema.”
AELEZA ANAVYOMFAHAMU LWAKATARE
Boniface Magessa alimuuliza hivi: “Ludovick, elezea kidogo unavyomfahamu Lwakatare. Siku ya tukio la kurekodiwa ulikuwa wapi? Kama mlikuwa wote siku hiyo, ulikaa mbele yake au nyuma yake?
Ludovick: “Magessa, Lwakatare tumekutana Bukoba 2010 wakati wa kampeni. Tumefahamiana kwa sababu ya Chadema tu. Na ameendelea kuwa rafiki yangu na kiongozi wangu.
Siku ya tukio la kurekodiwa nilikuwa nyumbani kwake Lwakatare. Siyo muhimu juu ya location”.
MASWALI MENGINE
Leila Sheikh alimuuliza hivi; “Ludo, eti uliwahi kuruka ukuta usiku fulani?
Ludovick: “Da Leilah umefunga wewe? Sasa haya ya kuruka ukuta usiku fulani ni nini tena? Teh teh, hebu fafanua? Marcois, siku hizi kibwagizo changu ni kuwa natazama yote haya nayo ni ubatili mtupu, ni sawa na kufukuza upepo”.
Swali lake lingine lilisomeka hivi: “Kama wewe ni mwanachama hai wa Chadema kwa nini umeitwa 'msaliti' na shabiki wa Chadema kuwa ile kanda ya Lwakatare ulitumwa na Mwigulu kuipiga? Je, ile kanda ni ya kweli?
Inadaiwa kuwa ile kanda inaonesha nia/mpango wa kumuumiza Msacky.
Katika majibu yake Ludovick naye alijibu “Leila, mimi ni Mwanachadema hai. Kuitwa msaliti ni hali halisi ya sasa. Lakini inawezekana kuwa mimi wanayeniita msaliti, siku moja wakaona kuwa ndiye mwokozi. Fikiria kama ningekuwa natumika kama mnavyosema, kwa nini kesi ya ugaidi imefutwa? Si ningesema tu kuwa kulikuwa na watu wengine kadhaa? Kama ninatumika, kwa nini nikamatwe Iringa na kusafirishwa usiku tena chini ya ulinzi mkali? Leila teh teh kwamba nilitumwa kurekodi ile kanda!!! Yaani na Lwakatare naye akatumwa ili aongee haya tunayotuhumiwa kuyapanga? Na je, suala hili ikionekana kuwa ni kweli Lwakatare alilifanya, nani atakuwa msaliti kwa Chadema? Je, chama chetu kinazo sera za kudhuru waandishi? Sasa msaliti ni yule anayechafua chama kwa kupanga mambo yasiyoendana na sera za chama? Au ni yule anaye kilinda chama? Haya si nyote mnajua concept ya whistle blowers? Hamtegemei wawemo ndani ya Chadema?
Na je, kama Mahakama itaamua kuwa tuhuma zetu ni kweli bila chembe ya shaka, ninyi mtaendelea kusema nini, kuwa mimi msaliti au wote sasa tutakuwa wasaliti? Naomba tuachie mahakama suala hili. Kuitwa msaliti wakati unaumia kwa ajili ya hao wanaokuita wasaliti, kibinadamu inaumiza sana. Na hilo ndilo linanitokea.
Kuhusu kwa nini watu wote wananilaumu, si kweli. Wapo wasioona hivyo, ila in a great party propaganda chafu za CCM na za Chadema zimenifanya muhanga wa mambo haya. Uhusiano wangu na Lwakatare kwa sasa ni wa mashaka sana.
Swali jingine la Sheila ni hili: “Je, wewe bado mwanachama wa Chadema? Kama ndiyo, mbona walikutema kwa muda ukakaa rumande bila dhamana? Kwa nini wewe ambaye ni volunteer wa Chadema ulikanwa pale baada ya kushikiliwa na polisi? Huo ndiyo u****wa kafara.
Alijibu hivi: “Mimi ni mwanachama wa Chadema na nakuhakikishia mateso yote ninayoyapata ni kwa sababu ya Chadema.
Masharti ya dhamana hayakuwa wadhamini wawekwe na Chadema, bali watu wawili. Sasa sidhani kama Chadema walikuwa na kesi mahakamani hadi watafute wadhamini. Kuhusu kuwa volunteer wa Chadema ni majungu niliyoyazungumza. Sijawahi kuwa volunteer wa Chadema. Mimi ni mwanachama wa kawaida.
Nyoni Magoha alimuuliza hivi: “Wewe bado una imani na Chadema? Utaendelea kuwa mwanachama hai au umeshajitoa/utajitoa?
Majibu ya Ludovick: “Ninayo imani kubwa sana na isiyotetereka kwa Chadema. Nitaendelea kuwa mwanachama hai”.
Hata hivyo, Ludovick ambaye anatajwa kuhusika na tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alikwepa kuzungumzia jambo hilo na hata alipoulizwa baadhi ya maswali yenye mwelekeo huo.
Kuhusishwa Ludovick na tukio la Kibanda kunatokana na utata wa kauli na mwenendo wake siku ambayo Mhariri Mtendaji huyo alijeruhiwa.
Kwa hisani ya Mtanzania
0 maoni:
Post a Comment