Wednesday 26 June 2013

Mrisho Ngassa aililia TFF

MSHAMBULIAJI Mrisho Ngassa amesema yeye ni mchezaji halali wa Yanga na siyo Simba. Ngassa alikuwa mchezaji wa kwanza kutangazwa kwenye usajili wa Yanga msimu huu akitokea kwenye kikosi cha Simba ambacho alikuwa akikichezea kwa mkopo kutoka Azam.


Hata hivyo, hivi karibuni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilisema kuwa bado halijapata mkataba wa Yanga na hivyo linamtambua Ngassa kama mchezaji wa Simba kwa sasa.

Ngassa alisema anawaomba TFF wamtambue kama mchezaji wa Yanga kwa kuwa ndipo mapenzi yake yalipo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ngassa alisema kuwa angeiomba TFF kumtambua yeye kama mchezaji wa Yanga na si Simba tena.

“Ninachojua mimi ni mchezaji wa Yanga. Sitaki kuzungumza mambo mengi sana kuhusu suala hili, lakini naomba TFF itambue kuwa mimi ni mali ya Yanga kwa sasa,” alisema Ngassa.

Usajili wa Ngassa umekuwa na utata mkubwa baada ya Simba nao kuibuka na kusema kuwa wana mkataba na mchezaji huyo.


Kwa hisani ya  Joan Lema / GPL

0 maoni: