Wednesday 26 June 2013

Ni kipi kinawapa ujeuri wabunge wa CHADEMA?

HAMY-D's Avatar
Wadau!
Katika historia ya nchi yetu Tanzania, hatukuwahi kupata wabunge wa upinzani wajeuri kama hawa tulionao sasa! Kwa mantiki hiyo hiyo ya ujeuri, wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakitumia lugha za matusi na zisizo za staha kwa viongozi waandamizi wa nchi (watawala). 
Na kwa mfano tu, ni ile kauli ya Mnyika ya kumwambia rais Kikwete ni dhaifu, pia Lema akaja na la kwake kuwa rais Kikwete ni muasisi wa udini, kwa sasa tunae Sugu na kauli yake kuwa Pinda ni mpumbavu!

Sasa jeuri hii wanaipata wapi hawa watu?. Je, ni kinga ya bunge?, au ni nguvu ya umma kama wanavyo jiaminisha ama ni mawakili walio bobea huko kwenye chama chao cha CHADEMA? 
Jeuri hii inatoka wapi?

Mdau HD

0 maoni: