Baada ya kusambaa kwa habari ya Zitto Kabwe kutaka kuanzisha chama kipya cha siasa, kupitia mitandao ya jamii mbalimbali Zitto mwenyewe afunguka na kusema .....
"Kwanza, Sina mpango wa kuanzisha chama cha siasa. Mimi ni mwanachama mwanzilishi wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16. Hiki ndio chama changu na chama cha familia yangu na kijiji chetu cha Mwandiga.-
Pili, nikichoka siasa nitafundisha, kuandika vitabu na kufanya tafiti. Sina muda wa kuanzisha chama kingine cha siasa na kuwachanganya tu Watanzania. Hivi sasa Watanzania hawataki utitiri wa vyama, wanataka mabadiliko. Wanataka huduma bora. Wanataka uwajibikaji wa viongozi wao kwao.-
Tatu, Hata kama ingekuwa ninataka kuungana na Watanzania wengine kuanzisha chama, nisingetegemea kwenda kukusanya nguvu Ujerumani. I hold western countries in contempt siku zote (ofcourse as a former marxist during students life this is expected).-
Mwisho watu waache kunisemea maana mwenyewe nipo naweza kujisema".
NB
Nitawawekea nilikwenda Ujerumani kufanya nini. Oh sorry ipo kwenye blogu yangu
Soma habari inayofanana na hii hapa chini
0 maoni:
Post a Comment