Saturday, 13 April 2013

Mama Sharo aanza kukomalia mali za mwanawe

MAMA mzazi wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, marehemu Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’, Bi. Zainabu Mkieti amefunguka kuwa kwa sasa anaanza kufuatilia haki za mwanaye kwenye kampuni alizokuwa anafanya nazo kazi kwani tayari ameshafungua mirathi.
Akichezesha taya na paparazi wetu kwa njia ya simu akiwa jijini Tanga, Mama Sharo alisema tayari ameshafungua mirathi na msimamizi ni mama mkubwa wa Sharo anayejulikana kwa jina la Fatuma Mkieti.

“Ndo tumeanza kufuatilia haki za mtoto wetu pia kujua benki alikuwa na fedha kiasi gani na jinsi ya kuzipata. Unajua hatukuona kabisa kadi ya benki ya Sharo, inawezekana ilipotelea palepale alikopatia ajali ila yote yatajulikana,” alisema mama Sharo.

Kwa hisani ya GLP

0 maoni: