Monday, 18 November 2013

Makahaba watumia ARV'S badala ya Kondomu

Madaktari nchini Kenya wameelezea wasiwasi kuhusu matumizi mabaya na ya kiholea ya dawa za dharura ambazo zinanuiwa kuwakinga waathiriwa wa ubakaji kutokana na maambukizi ya virusi vya HIV.
Dawa hizo zinazojulikana kama PEPS, zinapaswa kupewa mwathiriwa baada ya daktari kuthibitisha kuwa kweli yuko katika hali ya hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV, na hutolewa tu na wataalamu wa matibabu ya HIV. Lakini mwandishi wetu Zainab Deen aligundua kuwa wanawake makahaba wamegundua njia za kupata dawa hizo.
Kwa hisani ya BBC Swahili
Picha na kenyan2013

0 maoni: