Wednesday 6 March 2013

Siri ya Mapinduzi ya mapenzi ya WEMA na DIAMOND yafichuka

Penzi jipya

Kikulacho kinguoni  mwako .....Wema na Penny kumbe walikuwa mashostito?

SIRI ya Mtangazaji wa Televisheni ya DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ kumpindua Wema Isaac Sepetu kwa mwanamuziki Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ imevuja huku Wema mwenyewe akidaiwa kuchangia.
Mmoja wa marafiki wa Wema aliyeomba hifadhi ya jina alimtonya mwandishi wetu hivi karibuni kuwa, chanzo cha Penny kumnasa Diamond ni tabia ya Wema kupenda kumsifia sana Diamond kwa Penny huku akitoa siri asizostahili kuzianika kwa marafiki zake wa kike.


Alisema, Wema na Penny walikuwa marafiki (picha ukurasa wa nyuma zinathibitisha) na kwamba Wema alikuwa akimringishia mwenzake jinsi Diamond anavyojua kubembeleza na kumjali mwanamke na hapo ndipo mtangazaji huyo akafanya mapinduzi.

“Wema alikuwa  akimsifia Diamond kuwa anajua mapenzi na wanawake wengine wakishaambiwa hivyo huwa wanafanya wawezavyo kumnasa mwanaume huyo.



“Ndicho kilichotokea kwani alichokifanya Penny ni kumtega Diamond na hatimaye akamnasa. Ndiyo maana tunashauriwa kutowasifiasifia waume zetu mbele za marafiki zetu wa kike kwani ndiyo mwanzo wa kuibiwa,” alisema sosi huyo.


Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Wema kuzungumzia madai hayo lakini hakupatikana huku simu ya Penny ikiwa haipatikani.

Wema na Diamond wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu lakini katika siku za hivi karibuni Diamond amehamia kwa Penny. 


Angalia picha zaidi za Penny na Diamond

Full bata ....

Love on air!

Mambo ya kumpa support baby...... lol

Penny akiwa na Mama mkwe na rafiki wa Diamond

habari ndio hiyo full kula bata....

Habari na baadhi ya picha  hisani ya GLP

0 maoni: