Friday 1 February 2013

Mama Sharo Milionea afunguka ...Gari naliuza na Mimba ya Marry siitambui..

MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefunguka  na kuweka kila kitu bayana kuhusu gari aliloacha mwanaye pamoja na mimba ambayo inadaiwa ni yake.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Mama Sharo alisema: “Kuhusu gari lile Toyota Opa aliloacha marehemu mwanangu naliuza kwani siwezi kuliendesha na haliwezi kukaa bila kufanya kazi yoyote.
“Kwa upande wa Marry Lucas wa Sumbawanga msichana aliyejitokeza baada ya Sharo kufariki na kusema ana ujauzito wake, siwezi kumtambua kwa sababu enzi za uhai Sharo hakuniambia kuwa ana mchumba wala mpenzi.”  Baada ya kifo cha Sharo siku chache baadaye, Marry aliibuka na kudai alikuwa mpenzi wa Sharo na ana ujauzito wake.


0 maoni: