Friday 1 February 2013

Davina apiga Mkwara mzito kuhusu ndoa yake ........... asema watu wakomee


STAA wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ ameibuka na kusema watu wanaovumisha kwamba ameolewa mke wa pili wakome kwani yeye ndiye wa kwanza na wa mwisho kwa mumewe aitwaye Abdallah Shakoor. Davina ambaye siku si nyingi anatarajia kumzalia mumewe huyo alisema, amesikia watu wakichonga kuwa yeye ameolewa mke wa pili kitu ambacho si cha kweli.
“Nashangaa, haya maneno nilianza kuyasikia siku ya ndoa yangu kwani wambeya wasiopenda maendeleo ya watu walivumisha kwamba eti nimeolewa mke wa nne. Naomba wakome kabisa kwani mimi ndiyo wa kwanza na wa mwisho kwa Dullah,” alisema Davina.

0 maoni: