Friday 11 January 2013

Birthday ya Marehemu KANUMBA makaburini Mastaa vilio tupu


VILIO vimetawala katika kaburi la staa wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ (pichani)  baada ya baadhi ya mastaa kushindwa kujizuia na kumwaga machozi kutokana na kukumbwa na simanzi. Tukio hilo lilitokea Januari 8, mwaka huu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar baada ya wasanii wa filamu kuzuru kaburi la staa huyo katika siku ya yake yakuzaliwa.
Wasanii  walioongoza kumwaga machozi ni pamoja na Blandina Chagula ‘Johari’ na Mayasa Mrisho ‘Maya’ ambao waliungana na marafiki na wana familia kumkumbuka staa huyo kwa kuweka maua, kadi na  kuwasha mishumaa kaburini na kumuombea kwa Mungu.


Baada ya kutoka makaburini waombolezaji hao walikwenda katika Kituo cha Watato Yatima cha CHAKUWAMA kama alivyokuwa akifanya Kanumba kila mwaka katika siku yake ya kuzaliwa.


Katika kituo hicho kilichopo Sinza jijini Dar, wasanii, wanandugu na marafiki waliungana na watoto yatima na kuwapatia chakula pamoja na mahitaji mengine.

Akizungumza na Ijumaa mdogo wa marehemu, Seth Bosco alisema ataendelea kumkumbuka Kanumba na kufanya kila jema alilokuwa akilifanya.

Mbali na Johari na Maya, Chopa Mchopanga na Kadadaa walioshiriki, wasanii wengine wa filamu walikacha kuungana na familia kumuenzi Kanumba katika siku yake hiyo ya kuzaliwa huku mama mzazi wa marehamu, Flora Mtegoa akiwa Bukoba akimuuguza  mama yake.


Kwa hisani ya GPL

0 maoni: