Habari zenu wapenzi wa Hot n town
Natumai mu wazima na kama ilivyo ada mwaendelea vizuri na maisha ya kila siku, Leo nimeona si haba kama nikijaribu kuvitaja baadhi vijitabia au vidalili vinavyojitokea kwa baadhi yetu baada ya kupata penzi jipya.... ukiona dalili au tabia hizi jua "unasalitiwa"
1.Nakupenda lakini Sina Hisia nawe(Kwa wale ambao bado hawajaoana) Hii ni dalili kwamba Mpenzi wako ana mtu mwingine nje na inawezekana kabisa kwamba yeye ndo anapendwa zaidi yako wewe hata kama muda mwingi upo nae!.......ukiona hivi jua unatumika tu chanja mbuga!
2.Sisi ni Marafiki tu! (Kwa ambao bado hawajaoana) Ukimuuliza Mpenzio unanichukuliaje au mimi ni nani kwako anakuwa anasuasua...... Na kwa wale walio kwenye Ndoa ukiuuliza vipi mbona nakuona una mazoea ya karibu sana na mtu fulani? Utaambiwa ni Rafiki tu au mbona unaishi kwa hisia hujiamnini?!
3 Nahitaji muda wa kufikiria kuhusu hisia zangu! Hili nijibu tosha kwamba hana ukakika na penzi lake kwako ... na ujue wazi Kuna Mwenzio ambaye anamchanganya kiasi cha kushindwa kujijua kabisa .................hapo sio sehemu ya kukaaa ...... Anza kukaa tayari au mguu nje, mguu ndani!
4.Mabadiliko ya Ratiba za Kazi Kwa wale ambao wapo ndani ya ndoa au mahusiano ya muda mrefu, utaliona hili, mara kurudi late sana, ubize umekuwa mwingi mno hadi weekend! Na dharula za kikazi zisizoisha!!!!! hii imekula kwako...
5. Kutumia Muda Mwingi katika Computer Kama ameweza kujizuia kutoka toka hovyo, basi anaweza kuwa mtumiaji mzuri na wa muda mrefu wa Computer, atakaa hapo ata chat na kuongea na wezi wako tani yake, na unaweza usilijue hili kwani atakuambia ana kazi za ofisini anamalizia!aaaaaaah kaa chonjo hayo ni mambo ya Facebook na Twitter au Instagram basi hapo ukimuangalia sana haishi tabasamu....ndio ujiulize kazi za kazini zitamfanya aweke tabasamu?
6. Simu za Siri, Simu full mipassword utafikiri mtunza fedha wa halmashauri!!! Siku hizi simu zimekuwa nyingi, za usiku, mara simu ikipigwa ananyanyuka kwenda chumbani au kujificha kidogo, mara simu ikipigwa inakwatwa! Na ya kufanana na hayo!
7. Tabia yoyote yenye kutia Mashaka! Waswazi wanasema "Wasiwasi ndo Akili" Basi wasiwasi wako huenda ukakupa akili juu ya nini kinachoendelea na ukapata njia ya kuubaini ukweli! Ukiyaona haya au ya kufanana na haya kaa ukijua kuna kidudumtu kinawala na kitawatenganisha, Ni vyema ukachukua hatua! Pia Jiandae Kudanganywa!
.....................Stay tune .......................
0 maoni:
Post a Comment