ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe.
Hapa akionekana katika moja ya mikutano yake alipokuwa Karatu mkoani Manyara, inasemakana kuwa Askofu Geordavie hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, na mara zote huwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.
Mbali na kumiliki chopa ambayo ameinunua , askofu huyo huambatana na msururu wa magari yenye thamani kubwa kwenye mikutano yake kiasi cha kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.
Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.
Baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.
“Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.
Waumini wengi wamelalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka kumuona mtumishi huyo kutokana na ulinzi mkali anaopewa, Imefahamika kuwa utajiri wake hakuna mfano na nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud,”
0 maoni:
Post a Comment