Tuesday 3 June 2014

Kuna Ukweli wowote katika hili?Tabia ya Waandishi wa habari kuwa-blackmail watu mitaani?

Imezuka tabia chafu miongoni mwa waandishi wa habari ya kuwa-blackmail watu mitaani. Juzijuzi mwandishi mmoja (jina nalihifadhi kwa sasa) alitaka apewe Shilingi milioni 2 na ndugu yangu ili asiandike habari zake alizodai ni ‘mbaya’. Mwandishi huyu mshenzi alijitambulisha kuwa anatoka kwenye gazeti ambalo mhariri wake ni rafiki yangu. Nilipompigia simu mhariri na kumuuliza iwapo ana mwandishi anayeenda kwa jina hilo alisema huyo huwa anachangia tu makala kwenye gazeti lake na sio mwajiriwa. Alishangaa sana nilipomueleza kisa kizima, na alishauri tumuwekee mtego. Ana bahati sana mshenzi huyu! Nimeambiwa wapo waandishi wa habari wengi ‘feki’ wanaojihusha na mchezo huu mchafu. Nasema ole wao! Nafanya mawasiliano na Jukwaa la Wahariri na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ili, pamoja na mambo mengine ya kusimamiaa taaluma, waweze pia ku-deal na washenzi wa aina hii wanaochafua sifa nzuri ya wanahabari.

Uncle .FK Dar es salaam

0 maoni: