Saturday 29 March 2014

Umaarufu kazi: Mkongo aliyewagombanisha Wolper na Husna huyu hapa.... Siri zao za Kimapenzi zaanikwa, Yadaiwa Wolper ni zaidi ya Husna!

Mambo hadharani! Kigogo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayewagombanisha mastaa wawili Bongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid ni huyu hapa.... Anaitwa Rajab Mwami Shamweshi. Habari zilizolifikia Ijumaa zilidai kwamba baada ya mtafaruku wa mastaa hao kuripotiwa na gazeti mama la hili, Uwazi la Jumanne iliyopita, jamaa huyo aliibuka na kuanza kulalamika kwa watu wake wa karibu kuwa anachafuliwa mitandaoni kwa sababu ya mastaa hao. 
PATCHOU MWAMBA NDANI

Ilidaiwa kuwa Mwami alichukizwa na ishu hiyo kwani ilimhusisha mwanamuziki wa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye pia ni mwigizaji, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ kuwa ndiye humkuwadia kwa mastaa.

TUANZE NA PATCHOU

Kabla ya kumpata Mwami mwenyewe, Ijumaa lilizungumza na Patchou uso kwa uso amba alifunguka anachokijua juu ya sakata la Wolper na Husna kumgombea mwanaume huyo.
Alisema: “Mimi nashangaa kuona nachafuliwa mitandaoni lakini ukweli anayefanya hivyo ni Husna.

“Huyo Husna ni kweli aliwahi kutoka na Mwami lakini baadaye alimdharau Mwami kwa sababu alimuona hana pesa.

“Baada ya kuona pesa zimemtembelea Mwami akataka kurudi ndipo akakuta jamaa ameshajiweka kwa Wolper. Hapo ndipo Husna akaanza kuchanganyikiwa.” Patchou aliendelea kuweka wazi kwamba yeye na Mwami ni mtu na rafiki yake na pia ni ‘mapatna’ kwenye biashara.
Alisema amekuwa akikutana naye mara kwa mara Nairobi, Kenya na ndiye aliyemleta Bongo kwa ajili ya kuanzisha kampuni ya michezo ambapo alifikia hotelini.
KUWADI?

Alitiririka kwamba hajawahi kumkuwadia mwanamke lakini anachojua Mwami ni anajuana vizuri na Wolper kwani alimtambulisha walipokutana Nairobi hivi karibuni ndipo akaujua uhusiano wao.
Patchou: “Nilishangaa kwa sababu baada ya Mwami kutua tu Bongo, wasichana wa mjini walipojua  ndipo wakaanza kumsaka hadi chumba alichofikia hotelini.“Wengine walidiriki hata kumtumia picha za utupu ili kuwa naye kimapenzi baada ya kupata namba yake.” Patchou alisisitiza kuwa yeye si kuwadi kama wanavyomtangaza kwani hata huyo Wolper alishtukia amekutana naye Nairobi wakiwa na Mwami kwani kabla ya hapo alikuwa hajuichochote. Baada ya kumaliza kutoa utetezi wake, aliombwa kumpigia simu Mwami na kumuweka loud speaker  (sauti ya juu) ambapo alimweleza Mwami kila kitu ndipo akakubali kuzungumza na wanahabari wetu akiwa London, Uingereza.

KIGOGO AFUNGUKA

Akizungumzia sakata hilo, Mwami ambaye anadaiwa kuwa na ‘mihela’ hivyo kujitwalia taito ya ukigogo alisema kuwa anamfahamu Husna kama mtu wa kawaida ambaye aliwahi kufahamiana naye.

KUHUSU WOLPER

Kwa upande wa Wolper alisema kuwa anamfahamu kwa kumsikia na kumuona lakini si kimapenzi kama wanavyomchafulia jina. “Nilipokuja Tanzania kwa mara ya kwanza nilifikia hotelini…(anaitaja), kama wanavyodai hata chumba ndicho chenyewe lakini sikuja kwa ajili ya starehe za kimapenzi na wanawake, nilikuja kwa biashara zangu, nashangaa kuona nawekwa mitandaoni hovyo na anayeniweka namfahamu. “Naomba nisizungumze sana, niishie hapo nikirudi Tanzania nitaongea nanyi kwa uwazi kabisa,” alisema Mwami.

FUMANIZI

Wolper na Husna ambao waliwahi kuwa mashosti walianza manenomaneno hivi karibuni ambapo awali haikujulikana chanzo hadi pale Husna alipoamua kulifungukia hilo la mwanaume.

Ijumaa lilifanya jitihada za kumsaka Wolper kupitia simu yake ya mkononi, alipopatikana alisema angefika ofisini kwetu kutoa ufafanuzi lakini mpaka gazeti linakwenda mtamboni alikuwa hajafika na alipotumiwa sms ya kuulizwa kama angefika au la hakujibu.
Kwa hisani ya GPL

0 maoni: