Monday 31 March 2014

Ongezeko la joto lazidi kuwa tishio

Mafuriko kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
Mabadiliko ya tabia nchi duniani huenda yakaleta madhara makubwa zaidi na ambayo hayawezi kurekebishika, ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya. Wanasayansi na maafisa wanaokutana nchiniJapan wamesema ripoti hiyo imefanya uchunguzi wa kina kwa sasa kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi duniani.
Wajumbe wa jopo la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya hali ya hewa, wamesema ripoti hiyo inatoa ushahidi wa kutosha wa kiwango cha madhara hayo.
Mifumo asilia kwa sasa haufanyi kazi sawasawa, lakini ongezeko la madhara kwa binadamu ndilo jambolinalohofiwa zaidi.
Afya zetu, makaazi, chakula na usalama vyote viko katika hatari kutokana na kuongezeka kwa viwango vya joto, ripoti hiyo inasema.
Ripoti hiyo ilipitishwa baada ya majadiliano ya kina yaliyodumu kwa wiki moja mjini Yokohama.
Kwa hisani ya BBC Swahili

0 maoni: