Jean na Sarah walipatikana wakiwa wameuawa nyumbani kwao
Mwanamume mmoja anayeugua Saratani nchiini Uingereza, amefungwa jela maisha baada ya kumuua mkewe na mtoto wake msichana kutokana na athari za madawa anayotumia kwa matibabu ya Chemotherapy. Peter Redfern alimnyonga mkewe kabla ya kumshambulia kwa shoka na kumuua mtoto wake msichana Sarah katika mtaa wa Wath-upon-Dearne mwaka jana.
Redfern, mwenye umri wa miaka 70, alihukumiwa kifungo cha miaka 17 baada ya jaji kusema kuwa ni adhabu ya kutosha ambapo Redfern huenda akafa akiwa jela.
Alikiri kosa la mauaji ya mkewe na mtoto wake.
Miili ya Bi Redfern na mwanawe Sarah, ilipatikana baada ya Redfern kupigia simu polisi na kuwaambia kuwa amewaua mkewe na mwanawe.
Wawili hao walipatikana wakiwa wafunikwa nyuso zao kwa karatasi za plastiki
Sheffield anaugua aina ya Saratani ya mifupa ambayo haina tiba na ugonjwa wake uligunduliwa Mei mwaka 2013 na alikuwa amekubali kushirikishwa kwenye utafiti wa matibabu ya mchanganyiko wa dawa maalum kujaribu kumtibu.
Jaji alimwambia kuwa dawa alizokuwa anatumia ziliweza kuathiri fahamu lakini sio kwa kiasi kikubwa cha kumfanya kuwa muuaji.
Redfern wakati wote alikuwa analia jaji alipomkumbusha matukio ya mauaji hayo. Hata hivyo jaji alimwambia kuwa alifanya mauaji hayo akiwa mwingi wa fahamu kwani aliyapanga mwenyewe.
"Wakati Sarah alipowasili nyumbani, ulimkaribisha kwa karatasi ya plastiki na shoka vyote ulivyotumia kumuua. Na ulipogundua kuwa mtoto wako alikuwa ameshuhudia mauaji hayo, naye pia ukamuua ,'' alisema jaji
Hata hivyo jaji alipokuwa anatoa hukumu, alizingatia ugonjwa wa mshitakiwa ndiposa akaamua kumfunga miaka 17 jela. Na pia alisema kuwa kama isingekuwa ugonjwa wake pamoja na athari za dawa anazotumia, huenda asingefanya kitendo kama hicho.
Redfern alikiri kufanya mauaji hayo.
Kwa hisani ya BBC SWahili
0 maoni:
Post a Comment