Monday 24 December 2012

Uongo mwingine i nomaaaa!

Jamani jamani mambo mengine haya mtakuja kuaibika mtaani bure! yaani siku hivi watu bila kudanganya hawaoni raha.... sijui kwa nini lakini utakuta mt anakubali kuishi maisha sio yake kisa sifa au anataka kufanana na fulani, kwani ukiwa wewe  i mean ukiwa mkweli utakufa hebu soma hii? 

Jamaa:unasoma?
Demu:sisomi,vipi wewe unasoma?
Jamaa:ndio nipo kidato cha nne roleto.
Demu:jamani hiyo si ni shule ya wasichana?
Jamaa:aaah nimechanganya nipo ngaza 
Demu:mweeembona nayo ya wasichana 
Jamaa:ha! ha! ha! nilikuwa nakutania tu nachukua masters VETA.
Demu:mh ina maana VETA imeanza kutoa masters?
Jamaa:ishia zako demu mwenyewe hulipi wala nini unaniuliza maswali kama tuko uhamiaji? Kwa taarifa yako nipo CBE nasomea udaktari wa mifupa .........

0 maoni: