Friday 20 December 2013

Baby Madaha azidi kumponda Diamond... asema akawatishie watoto wenzie wa Tandale

MWIGIZAJI na mwanamuziki Bongo, Baby Joseph Madaha amemchana Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kumwambia awatishie watoto wa Tandale kwani hana ubavu wa kuchuana naye. Akizungumza na paparazi wetu, Baby alifunguka kuwa anamshangaa Diamond kujibu kuhusu jinsi alivyomchana wiki kadhaa zilizopita gazetini na kusema yeye hamuwezi kwani alimtangulia kuchomoka kistaa.

“….akiwa bado ana-struggle kupata mkwanja awatishie watoto wenzake wa Tandale, mimi nishazindua brand yangu ya manukato na mikoba ya zawadi, bidhaa ambazo zinaingia sokoni rasmi Desemba 31, awatishe haohao watoto wenzake, mimi siyo saizi yake,” alisema Baby. Diamond alipotafutwa, simu yake iliita bila kupokelewa.
Kwa hisani GPL

0 maoni: