Monday 18 November 2013

Kuna ukweli wowote katika hili?

Wanajamvi,
Juzi tarehe 13/11/2013 mida ya saa tano usiku, nilipigiwa simu kwa namba +4915739568962 nikaambiwa nikae tayari kwa kifo wakati wowote, Mtu huyo akaendelea kusema najifanya mjuaji Sana, nimwambie alinilia nini? Aliongea mengi lakini mwisho akamalizia kwakusema, nitakuonyesha kuwa mimi natoka Kigoma.

Kwahekima kabisa mimi nilipuuzia madai hayo hasa baada ya mwanasheria wangu kunishauri nipuuze,

Lakini Leo majira ya alasiri nimepokea barua pepe kutoka kwa msemaukweli868@gmail.com

yenye madai yanayofanana na ya juzi kwenye simu juzi, na Leo ikasisitizwa kuwa ananipa saa 48 za kutenganisha uhai wangu,

Baada ya hapo familia yangu na mwanasheria wakashauri tufungue kesi polisi,

Tumefungua polisi kesi kwa KGD/RB/9833/2013

Mimi kama mlalamikaji nimeulizwa kuwa nani ninaemuhisi kwa tukio hili? Nikajibu Ni Zitto Zuber Kabwe.

hivyo maelezo polisi yamesimama hivyo,

Taratibu za kipolisi zinaendelea 

Nashukuru jeshi la polisi Dar hasa mkoa WA kipolisi Temeke,

Nataka kesi hii iwe mfano kwa wanasiasa wanaotumia nafasi zao za kisiasa kutishia na kudhuru raia wasio na dh


Kwa hisani ya Y.N

0 maoni: