ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Yanga SC, Jamal Malinzi amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27, mwaka huu. Fomu hizo zilianza kutolewa juzi. Jumla ya wagombea 25 katika nyadhifa mbalimbali wameshachukua fomu.
Taarifa iliyotumwa jana na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, ilisema ukiachana na Malinzi, mwingine aliyejitokeza katika nafasi ya urais ni Omari Nkwarulo, wakati kwenye umakamu wa rais kuna Wallace Karia na Ramadhani Nassib.
Wambura alisema waliochukua fomu za ujumbe ni Athumani Kambi, Charles Komba, Davis Mosha, Elias Mwanjala, Eliud Mvella, Epaphra Swai, Farid Nahdi, Hussein Mwamba, Jumbe Magati, Kamwanga Tambwe, Khalid Mohamed, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Omari Walii.
Wengine ni Samwel Nyalla, Shaffih Dauda, Stanley Lugenge, Twahir Njoki, Vedastus Lufano, Venance Mwamoto na Wilfred Kidao.
Kwa upade wa Bodi ya Ligi, aliyechukua fomu ni mmoja tu ambaye ni Hamad Yahya, anayeomba kuwania uenyekiti.
Wakati huohuo, Wambura amesema mechi ya Ngao ya Jamii iliyozikutanisha Yanga na Azam juzi, imeingiza Sh milioni 208 zilizotokana na kuhudhuriwa na mashabiki 26,084.
Kwa hisani ya Hans Mloli/GPL
0 maoni:
Post a Comment