Friday 30 August 2013

Kumbe ndio mchezo wake! Aliyempiga Chupa AUNT EZEKIEL ndiye aliyemchana LULU Viwembe

Yvonne
IMEVUJA! Mtuhumiwa aliyempiga chupa mwigizaji Aunt Ezekiel Jumapili iliyopita nje ya Ukumbi wa Bilicanas ndiye aliyewahi kumchana viwembe mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwaka 2011.


Data za Ijumaa zinaonesha kuwa, mwaka 2011 Lulu alivamiwa na wadada wa mjini baada ya kunaswa katika pozi tata na mwanaume wa watu maeneo ya Kariakoo, jijini Dar. Alipoulizwa juu ya sakata hilo, Lulu alitiririka hivi: “Naweza kumkumbuka mwanamke mmoja, namfahamu kwa jina la Yvonne, alinivamia na kuanza kunishambulia huku mkononi akiwa ameshika wembe...”


Mwishoni mwa wiki iliyopita, Yvonne huyohuyo ndiye aliyedaiwa kumpiga chupa mkononi Aunt ambapo haikubainika mara moja sababu za kufanya tukio hilo. Aunt alipelekwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni na kushonwa nyuzi sita huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi.

Aunt Ezekiel

LULU


Kwa hisani ya Imelda Mtema/GPL


0 maoni: