Wadau naombeni ushauri.....
Mimi ni Mwanamke mwenye umri wa miaka 34 sijabahatika kuzaa na wala kuolewa ila kwa kipindi cha miaka 6 nimekuwa kwenye mahusiano na mwanaume mwenye mtoto mmoja aliyefiwa na mkewe miaka 7 iliyopita , tatizo lipo hivi..... Mimi na mpenzi wangu tulifanikiwa kuishi pamoja bila ndoa kwa muda wa miaka 5 ila kutokana na ugomvi wa kila siku na maneno maneno yasiyoisha niliamua kuhama na kupanga nyumba......Ndugu wa mwanaume na marafiki hawanipendi na mara zote huniongelea vibaya.....Wanadai mimi nipo kimaslahi zaidi , mlevi na jeuri .....
Cha ajabu wakati tuaanza mapenzi mpenzi wangu hakuwa na chochote na yeye ndie aliyehamia kwenye nyumba nilipokuwa nimepanga kwa gharama zangu ..... kwa sasa anamiliki nyumba, mashamba na viwanja kadhaa....... Ndugu zake na marafiki zake hao wasionipenda ndio walikuwa mstari wa mbele kuja kushinda nyumbani kwetu kipindi cha mapumziko na kuhudumiwa chochote wanachokitaka............ Baada ya mimi kuhama Ndugu na marafiki zake walizusha mengi na kusema kuwa mimi nimepata mwanaume aliyenifanya nimkimbie mpenzi wangu na waliongea haya bila kutoa ushahidi wowote..... Baada ya mimi kuhama mawasiliano yalikatika kabisa na hii ilitokana na maneno ambayo mimi na mpenzi wangu tulikuwa tukiyapata toka kwa ndugu na marafiki zetu.....
Baada ya kukaa mbalimbali kwa zaidi ya miezi 6 tuliamua kurudiana na kuanza upya, tulikaa chini na kupanga mipango ya kuwa na maisha pamoja na kusahau yote yaliyopita ingawa niligundua kuwa alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine aliyekuwa akimleta kwenye nyumba tuliyokuwa tunaishi pamoja, mwezi mmoja baada ya kurudiana mpenzi wangu alibadilika gafla akawa hapokei simu wala kujibu meseji zangu hadi leo na kuna tetesi kuwa ndugu zake wamemtafutia mwanamke aoe baada ya kupewa taarifa za mimi na yeye kurudiana, pia kumekuwa na vikao vingi vya kuweka mikakati ya mimi na yeye tuachane na familia yake imekuja juu kwa nini yeye anirudie?...... Nifanyaje? nimpe muda na kumpigania au nisonge mbele na maisha yangu?
Majibu yenu ndio maamuzi yangu - Aunt S Dar.
0 maoni:
Post a Comment