Monday, 22 July 2013

Sakata la Unga la Agnes Masogange makubwa yaibuka

ZIMEPITA siku 16 tangu Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kunaswa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo mjini Kempton Park nchini Afrika Kusini, mapya yameibuka kuambatana na tukio hilo, Risasi Jumamosi linakupasha.

Chanzo chetu cha ndani kilichoongea na paparazi wetu juzi jijini Dar, kimesema neno kwa neno, hasa matukio ya siku nne wakati staa huyo akijiandaa kuondoka nchini. Masogange aliondoka Julai 5, 2013.

JULAI 2, 2013

Masogange alipika pilau nyumbani kwake, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam na kuwaalika watu mbalimbali, wakiwemo kaka zake ambao majina yao hayakupatikana mara moja. Katika ‘hafla’ hiyo, Masogange alisema amejisikia kula pamoja na watu hao ili kutimiza furaha ya moyo wake. Hakusema ana furaha gani.

JULAI 3, 2013
Inadaiwa Masogange siku hiyo aliazima gari la mdau wake mmoja (jina tunalo) na kuwa nalo kwa saa kadhaa. Safari yake kubwa ilikuwa Sea View Hotel, jijini. Siku hiyo staa huyo hakuwa akipokea simu asizozijua. Wale aliowajua aliwaambia ana mazungumzo nyeti na mtu hotelini hapo, hivyo wapige baadaye.

JULAI 4, 2013 
Masogange aliposti picha kwenye Instagram akiwa yeye na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ wakila ‘bata’. Aliandika maneno mbalimbali kama; ‘libeneke la bata litaendelea nikirudi.’ Hakusema anakwenda wapi na lini atarudi.

KUHUSU ‘UNGA’
Chanzo kilisema: Nijuavyo mimi mtu akiwa na mabegi mengi yenye madawa ya kulevya na anataka kusafiri nayo, yanatangulia uwanja wa ndege. Hivyo naamini mzigo ulipelekwa uwanja wa ndege siku hiyo.

ALIKWENDA SALUNI
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, pia siku hiyo jioni alikwenda saluni moja iliyopo Sinza Madukani, Dar. Jina halijajulikana.

JULAI  5, 2013
Shuhuda anasema saa 4:06 asubuhi, Masogange alifunga safari kwenda uwanja wa ndege akiwa ameongozana na Melisa Edward ambaye anadaiwa kukamatwa naye siku hiyo.

MABEGI YANAYOTUMIKA KUBEBEA ‘UNGA’
Kingine ambacho kimesemwa, mabegi yanayotumika kubebea ‘mzigo’ ni spesho kwa kazi hiyo ambapo ndani yana zipu mbili. “Mabegi yaliyotumika siku hiyo si haya ya kawaida yanayouzwa na machinga, unajua wabeba unga wanatumia mabegi yanayojulikana kwa jina la Hand Curter, juu yana zipu moja kubwa, ndani kuna zipu mbili ambazo wewe kuziona ufanye kazi. “Begi moja linauzwa shilingi laki nne (400,000). Kama uwanja una zana duni za kukagulia, hawawezi kuona unga ndani,” alisema sosi huyo.

MZIGO ULITOKEA BARA LA ASIA
Kwa mujibu wa maelezo ya mtu mwingine, mzigo aliokamatwa nao Masogange unadaiwa kuingia Bongo Juni 29, 2013 ukitokea nchi moja iliyopo Bara la Asia (jina tunalo). “Sina uhakika na lini mzigo huo uliingia au safari hiyo aliipanga, lakini kumbukumbu zangu zinaniambia mzigo uliingia Bongo Juni ishirini na tisa, mwaka huu, ukitokea nchini …(anaitaja jina),” alisema mtu huyo.

AKIPATIKANA NA HATIA ADHABU NI HII
Habari kutoka chanzo chetu kimoja nchini Afrika Kusini, mtu anayepatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya kwa kuuza au kubeba huhukumiwa kifungo cha maisha au kifungo cha miaka 20.

MADAWA YAMEPELEKWA KWA MKEMIA
Aidha, kuna habari kwamba baada ya serikali kuyadaka madawa hayo, yamepelekwa kwa mkemia mkuu kwa ajili ya uchunguzi zaidi na majibu yatatolewa Agosti, mwaka huu. 

DHAMANA IPO WAZI, NANI AMUWEKEE?
Habari mbaya ni kwamba, dhamana ya Masogange na mwenzake iko wazi mahakamani lakini watu wa kwenda mstari wa mbele kumuwekea ndiyo wamekuwa wakiingia mitini. “Huku dhamana iko wazi, ila kila mtu anaonekana kukwepa kumdhamini. Sijui watu wanadhani atatoroka? Lakini nijuavyo mimi hawezi kutoroka kwa sababu paspoti yake inashikiliwa na serikali,” alisema mnyetishaji wetu aliye nchini humo.


Kwa hisani ya Shakoor Jongo/ GPL

0 maoni: