Friday 12 July 2013

Dida apigwa dongo


BAADA ya hivi karibuni Mtangazaji wa Radio Times, Khadija Shaibu ‘Dida’ kufunga ndoa na mwanaume aitwaye Ezden, mashosti zake wamemtaka kutulia sasa na asijaribu kugeuza ndoa kuwa fasheni. Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya mastaa walioomba hifadhi ya majina yao ambao walihudhuria ndoa hiyo iliyofungwa Ijumaa iliyopita Ubungo jijini Dar walisema, wamechoka na mialiko ya ndoa zake kila baada ya kipindi kifupi hivyo ni wakati sasa wa kutulia.

“Asifanye ndoa kama fasheni, tumechoka kuhudhuria sherehe za ndoa yake, kama ana kasoro, ajirekebishe ili atulie sasa ajenge maisha yake,” alisema staa mmoja ambaye ni rafiki wa karibu na ndugu wa Dida. Hata hivyo, akizungumzia kuhusu kuolewa huko, Dida alisema safari hii ndoa yake ikivunjika haolewi tena.


Kwa hisani ya Na Hamida Hassan /GPL

0 maoni: