Sunday 7 July 2013

Baada ya TID kuponda Wakazi ajibu mapigo



Rapper Webiro Wassira aka Wakazi ameamua kufunguka baada ya TID kumponda  kuwa haoni ataimba nini huko Afrika ya Kusini kwenye show ya Big Brother Africa The Chase kinaonesha kuwa staa huyo wa ‘Kiuno’ hajui anachokiongea.

Kupitia ukurasa wake wa  Twitter, TID aliandika hivi : Wakazi ataimba wimbo gani, anaenda kuonyesha kofia zake za marekani#mzeekasema#radarworththisshit
#watuwabaya#msiwemaf**a.

WAKAZI baada ya kupata ujumbe  alisema: Sasa ntamjibu nini, anaongea vitu asivyovifahamu, yeye hapo akimuona Wakazi anaona kofia za Marekani sasa mtu kama huyo utaongea naye!!”
“The greatest ignorance ya mtu ni pale anapoamua kudiss kitu ambacho hakijui au  ajakifahamu bado vizuri , mtu kama huyo huwezi kuanza kubishana naye, na yeye ananiona mimi Mmarekani, wakati mimi ni Mtanzania, angekaa miaka mitatu Ulaya au Marekani angejiona na yeye ni mtu wa huko kwa jinsi upeo wake ulivyo.”

0 maoni: