Wednesday 10 July 2013

Alfred Rwakatale wa Chadema alazwa?

Toka jana tarehe 9/07/2013 Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Kamanda Alfred Lwakatare (pichani) amelazwa hospitali ya Muhimbili......Nanukuu maelezo yake hapa
‘’Mkirejea tatizo la kiafya nililolipata nikiwa Central Police baada ya kukamatwa; la kuumwa sana na mgongo/mkono na baadaye nikiwa gerezani Segerea nilipelekwa Muhimbili Moi na baada ya vipimo (M.R.I) wakabaini kuna ulazima wa kufanyiwa upasuaji. Tatizo hili limeendelea na hata baada ya kutoka Segerea na nimekuwa nikiwaona madaktari kwa ukaribu. Jana mchana, imelazimu kulazwa hospitali ya Muhimbili ward ya Sewahaji NO.18,chumba No.024 kwa uchunguzi na matibabu zaidi. 

Kama ilivyo kawaida yetu; Tunaanza na Mungu,Tunaendelea na Mungu na kumaliza na Mungu.

Tuzidi kuombeana na yote tumkabidhi Mungu.
Nawapenda sana!’’



0 maoni: