Tuesday 11 June 2013

Kala Jeremiah atoa tuzo yake kwa Magwea......

Kupitia  ukurasa wake wa moja ya mtandao ya jamii Msanii bora wa Hiphop mwaka 2013 - Kala Jeremiah  ameandika hivi....
MIMI KAMA MSANII BORA WA HIP HOP KWA MWAKA HUU NAPENDA KUCHUKUA MUDA HUU KUWATANGAZIA WATU WOOTE KUWA. KATIKA TUZO TATU NILIZOCHUKUA MOJA NAIKABIDHI KWA ALBERT MANGWEA.YANI NI TUZO YA MANGWEA NA NITAIPELEKA KWA MAMA MZAZI WA MANGWEA MOROGORO.

NIMEAMUA HAYO KWA KUWA HAYATI ALBERT MANGWEA ALIKUWA ANAFANYA MZIKI AMBAO UKO UPANDE AMBAO MIMI NIMESHINDA TUZO TATU YANI HIP HOP.

TUZO NILIYOAMUA KUMPA MANGWEA NI TUZO YA MSANII BORA WA HIP HOP. KWA KUWA ALIKUWA ANASTAHILI PIA KUITWA HIVYO

TUZO HII NAAMINI ITAKUWA UKUMBUSHO MHIMU SANA KWA FAMILIA YAKE.LAKINI PIA ITAKUWA INAONYESHA MSHIKAMANO WETU KAMA WASANII WA HIP HOP.''

POPOTE ULIPO KAMA WEWE NI SHABIKI WA HIP HOP TAFUTA NJIA YOYOTE YA KUENDELEA KUMUENZI NDUGU YETU

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI HIP HOP.

0 maoni: