Monday, 20 May 2013

Sinema ya bure DIVA na PREZZO!

NGOJA nikutambulishe kwa mara ya kwanza kwa wasomaji wangu. Nazungumza na wewe Loveness Malinzi ‘Diva’. Ulianza ‘kuhaso’ kutoka kimuziki miaka ile ulipoibuka Nyumba ya Kukuza Vipaji (THT). Kabla ya kuchomoka kimuziki, ukala shavu la utangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM. Ndicho kimekupa jina kwa kuwa kinagusa hisia za kimapenzi.


Weka utangazaji pembeni, nakuzungumzia kama msanii wa Bongo Fleva. Wimbo wako wa Piga Simu uliomshirikisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiyo uliofanya mashabiki wako ambao hawakukufahamu kabla ya kuwa mtangazaji, kugundua kuwa kumbe una kipaji cha muziki. Utambulisho unatosha!


Wiki iliyopita uligeuka habari ya mjini. Ni baada ya kutangaza kuwa umetokea kumpenda ghafla (first sight love) mwanamuziki mwenye fedha wa Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ kama ilivyowahi kutokea kwa wengine uliowakaribisha studio. Ilikuwa ni baada ya kumkaribisha kwenye kipindi chako cha Ala za Roho kwa ajili ya mahojiano.

Umetambulisha utamaduni mpya kidogo kwa mabinti wa Kitanzania. Umevunja kasumba kuwa mwanaume ndiye humtokea mwanamke anapokuwa na hitaji la kimapenzi. Umeibua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii. Sakata lako limeonekana kama sinema ya bure. Unajua kwa nini? Kuna waliodai umewashushia heshima wanawake wa Kibongo kwa kujirahisisha kwa mwanaume. Kuna waliosema umempora mwenzako, Lady Boss aliyekuwa mpenzi wa Prezzo, ukawa gumzo nchi zote mbili, Tanzania na Kenya. 

Pamoja na kwamba ni mapenzi lakini kuna madai mazito kuwa kwa kufanya hivyo umemwachia maumivu aliyekuwa mpenzi wako wa Bongo. Pia umemsababishia maumivu makali mwanamke mwenzako, Lady Boss wa Prezzo, bila kujali kuwa wewe ni ‘mwalimu’ wa mapenzi kupitia kipindi chako.

Nikueleze tu wazi kuwa kinacholeta tafrani na matusi kutoka kwa baadhi ya watu mitandaoni ni kwa kuwa huachi kumsifia na kueleza jinsi ‘unavyo-mmisi’ kama ulivyokuwa ukifanya ulipokuwa na uhusiano na rapa wa hapa nyumbani, Mo Racka. Watu wanadai tatizo lako ni kulinadi penzi hilo jipya bila kujali walioumia.

Sawa umempata Prezzo, umetukanwa vya kutosha, ombi letu, tulia ili kujenga heshima kwa wanawake wa Kitanzania wanaopata wanaume nje ya Bongo. Usiwe kama wale walioolewa na wazungu ‘vibabu’ kwa tamaa ya fedha. Unachotakiwa kufanya ni kuwathibitishia wale wanaodai kuwa umefuata mkwanja wa Prezzo kuwa si kweli bali una mapenzi ya dhati kutoka moyoni na siyo ya mapenzi ya matangazo. Kila la kheri katika maandalizi ya ndoa. For the love of game!


Kwa hisani ya GLP

0 maoni: