Wednesday 15 May 2013

Mashetani yavamia shule ya Sekondari Manzese

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam jana wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda maeneo hayo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.

Angalia picha zaidi hapa chini






Picha - Zainab Chondo -ITV

0 maoni: