KUTOKANA na ndoa za mastaa wengi kuvunjika, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Sunday Mangu ‘Linex’ amefunguka kuwa japokuwa ana mchumba hayupo tayari kuoa kwa fasheni kwa kumuiga mtu f’lani kwani anaogopa kuharibu dira nzima ya maisha yake.
Akichezesha taya na paparazi wetu juzikati, Linex alisema kwa sasa yeye na mchumba wake Mzungu aitwaye Suvi Rikka(pichani) bado wanasomana na kila mmoja akisharidhika na tabia ya mwenzake ndipo suala la ndoa litafuata.
“Mimi sitaki kuoa kwa fasheni eti kwa kumfuata mtu f’lani na sitaki kufunga ndoa leo halafu kesho imevunjika, nataka mimi na mke wangu tuishi milele,” alisema Linex.
Kwa hisani ya GLP
0 maoni:
Post a Comment