Monday 1 April 2013

Shilole afunguka baada ya kuwekwa mtu kati

Wiki iliyopita katika safu hii tulimtambulisha kwenu msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kama kawaida maswali mengi yaliulizwa kama ifuatavyo:
KWELI ALIOLEWA?
Eti ni kweli uliolewa na ulikuwa unaishi Keko? Khatibu, Dar, 0715456296.

SHILOLE: Kweli.

TABIA YA KUTONGOZA SERENGETI BOYS
Shilole acha kutongoza watoto wadogo halafu sauti ya kuimba huna, acha fani za watu. Sister Havinitishi, Dar, 0655196161.

SHILOLE: Mimi kwanza ni mdogo na siwatongozi watoto wadogo, kuhusu kuimba nitajifunza zaidi.

KUHUSU BABA WATOTO WAKE
Dada Shilole uko juu nakupa big up! Ningependa kufahamu hao watoto wako umezaa na baba mmoja au kila mtoto ana baba yake? Angel, Dar, 0714600415.

SHILOLE: Asante, watoto wangu kila mmoja ana baba yake.

HUYU AMEMZIMIA
Shilole naomba namba ya simu maana unanikosha wewe ni mzuri sana. Sangoti, Korogwe, 0654848387

SHILOLE: Asante, nitakutafuta.

KUHUSU MIDUME MCHARUKO MTAANI
Shilole wewe ni msanii mahiri kunako kiwanda cha filamu na muziki Bongo, je, unajiepusha vipi na midume inayokutokea kimapenzi? Salim Liundi, Dar, 0658110395.

SHILOLE: Asante, huwa najiepusha na midume kwa kujiheshimu na kujilinda hivyo siwapi nafasi.

UHUSIANO WAKE NA NGASSA
Shilole nataka kujua eti wewe na kiungo mahiri wa timu ya Simba Mrisho Ngassa mnatoka kimapenzi, mbona kuna tetesi za ajabu kitaani? Msomaji.

SHILOLE: Siyo kweli.

MZAZI MWENZAKE VIPI?
Umesema una watoto wawili, je vipi kuhusu mzazi mwenzio uko naye au ndiyo umemtema baada ya kupata umaarufu? Shariff Juma, Dar, 0713332349.

SHILOLE: Siko naye.

BIFU LAKE NA FLORA
Shilole hongera kwa kazi zako unajitahidi ila nataka kujua kwa nini hupatani na Flora Mvungi.  Silla, Dar, 0718764242.

SHILOLE: Asante, mimi sijagombana na mtu ila mti wenye matunda siku zote lazima upigwe mawe.

KUFICHA WATOTO WAKE
Zamani ulikuwa unaficha kama una watoto wawili mpaka mtu wako wa karibu alipotoa hiyo siri, kwa nini ulifanya hivyo? Cassian, 0655202202.

SHILOLE: Siyo kweli mbona watoto wangu wapo wazi!

KUHUSU MKOROGO
Big up! Shilole napenda muziki wako ushauri wangu kwako acha mkorogo unakuharibu. Tina, Mwanza, 0719747965.

SHILOLE: Siku hizi sipaki mkorogo, nimeacha.

SKENDO YA KUTOKA NA RAY
Dada Shilole unafanya kazi nzuri ila punguza skendo nasikia ulishawahi kutembea na Ray, je ni kweli? Charles Mallya, Mwanza, 0759022399.

SHILOLE: Asante, sijawahi kutembea na Ray.

BARNABA JE?
Shilole hivi ni kweli ulikuwa unatembea na Barnaba na kwa sasa mpenzi wako ni nani? Musa Mbughi, Sumbawanga, 0764021259.

SHILOLE: Siwezi kusema chochote.

UKWELI KUHUSU KUBAKWA
Shilole najua mtoto wako wa kwanza umezaa na Makala wa Igunga Tabora na ulikuwa unaishi naye kwa Tatu Balozi, ilikuwaje ukasema mwanaume aliyekupa mimba ya kwanza alikubaka? Ibrahim Yusuph, Dar, 0719599195.

SHILOLE: Sipendi kurudi nyuma ila ni kweli alinibaka nikapata ujauzito.

HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Dada nataka kujua historia yako kiufupi. Sultan, Dar, 0654324222.

SHILOLE: Nimezaliwa Igunga Tabora nikiwa mtoto wa mwisho, sanaa nilianza mwaka 2010.


Kwa hisani ya GLP

0 maoni: