Sunday, 10 March 2013

Serikali yaingilia kati sakata la JACK WA CHUZI kujiuza...

BAADA ya hivi karibuni msanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kunaswa akipelekwa kuuzwa kwa mwanaume, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos  Makalla anadaiwa kuicharukia skendo hiyo ambapo juzikati alimvaa Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon Mwakifwamba na kumuuliza juu ya tukio hilo la aibu. 
Chanzo cha habari kutoka ndani ya shirikisho hilo kilitonya kuwa, Mhe. Makalla alimvaa Mwakifwamba kwenye mkutano na wasanii uliofanyika ndani ya Hoteli ya Kibadamu, Ubungo jijini Dar.


“Mhe. Makalla ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, akiwa pale alimuuliza Mwakifwamba kuhusu hatua walizochukua kwa Jack Chuzi baada ya kuandikwa habari kuwa alinaswa akienda kuuzwa.



“Mwakifwamba alijitetea kuwa, wanalishugulikia na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Michael Sangu ‘Mike’ akasisitiza kuwa, wako katika mchakato wa kulitolea uamuzi tukio hilo lililofanywa na Jack ,” kilidai chanzo hicho.


Baada ya kuzinyaka habari hizi Mwandishi wetu alimtafuta Mwakifwamba lakini hakuweza kupatikana mara moja ila Mike alipoulizwa juu taarifa za Mhe. Makalla kucharukia ishu ya Jack alisema:



“Ni kweli waziri aliuliza kuhusu hatua tulizozichukua kuhusu suala la Jack kujiuza ambapo nilimjibu kuwa tuko kwenye mchakato wa kulitolea uamuzi na kwa sasa tumeunda kamati maalum, ikimaliza uchunguzi wake ndiyo tutatoa jibu kuwa tumemchukulia hatua gani.”

0 maoni: