Friday 1 March 2013

Qeen SUZZY na G- SEVEN wamwagana..........

ULE uchumba uliodumu kwa muda mrefu wa mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ na aliyekuwa rapa wa bendi hiyo, Aimerichad Mwamba ‘G-Seven’ umevunjika na sasa kila mtu ana maisha yake.

Chanzo makini kilicho karibu na Queen Suzy kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitunyetishia kuwa, uchumba huo ulivunjika siku nyingi lakini mwanadada huyo alikuwa akifanya siri akijua taarifa hizo zikivuja ataaibika.
Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo, Ijumaa lilimtafuta Queen Suzy kuzungumzia hilo alipopatikana alisema: “Ni kweli mimi na G- Seven siyo wachumba tena na sababu ni kukosekana uaminifu, wanaomtaka wamchukue tu.”

Kwa hisani ya GLP

0 maoni: