Kutoka mbegu za kiume muda mfupi baada ya kumwingilia mwanamke huitwa premature ejaculation. Huu ni udhaifu wa kawaida kwa wanaume walio wengi kwa ujumla wake, ikiwa ni pamoja na vijana. Mtaalamu Ira Sharlip anasema katika utafiti wake kuwa, ni kiasi cha asilimia 20 hadi 30 ya wanaume wa rika zote ambao wana matatizo haya.
Njia za kitabibu za kuweza kumtambua mtu mwenye udhaifu huu inaitwa Intravaginal ejaculatory latency time(IELT). Hata hivyo, mtaalamu Ira Sharlip anaongeza kwa kusema kwamba, utaratibu huu hausaidii sana kumjua mtu mwenye premature ejaculation. Kuna wanaume ambao wanamaliza katika dakika moja tu baada ya kumwingilia mwanamke na wao hudai kwamba, hawana matatizo.
Na halafu upande mwingine, kuna wanaume ambao wanaweza kuchukua dakika 20 bila kutoa mbegu baada ya kumwingilia mwanamke. Hawa nao ni wagonjwa, kwani muda huo ni mkubwa kuliko wastani. Kwa maana nyingine ni kwamba, maana ya neno premature, zaidi zaidi liko katika mtazamo wa mhusika mwenyewe. Inategemea na mtu mwenyewe anavyotosheka kimapenzi na uwezo wake wa kujidhibiti muda wa kumaliza unapokuwa umewadia.
Utafiti wa mwaka 2010 katika jarida la Journal of Sexual Medicine uliona kwamba, kipimo kizuri cha premature ejaculation ni dakika 5.4. Yaani mtu akitoa mbegu baada ya dakika pungufu ya hizo, tangu amwingilie mwanamke basi ana ugonjwa huu wa premature ejaculation.
Lakini Ian Kerner anasema kipimo ni dakika mbili. Yaani mwanaume akimaliza haja yake kabla ya dakika mbili, basi ana ugonjwa huo. Anaongeza kwamba, watu wengi anaokabiliana nao ni wale ambao wanatumia muda mfupi chini ya dakika mbili kumaliza haja zao. Wengine hutumia sekunde 30 tu!
Pia hata sababu za nje zinaweza kuchangia kumfanya mwanaume akawa na tatizo hili. Mtu mwenye mawazo mengi ni rahisi kukumbwa na tatizo hili. Mtu mwenye mawazo mengi anamaliza haraka mara baada ya kumwingilia mwanamke, kwa mujibu wa mtaalamu Kerner.
Lakini kumaliza kwa namna hii pia kuna uzuri wake kwamba, tumejaza dunia kwa kuwa na watu wengi. Kama watu wangekuwa wanachukua saa nzima kumaliza baada ya kumwingilia mwanamke, dunia ingekuwa na uadimu wa watu!
Washauri nasaha wanaojihusisha na ushauri wa kimapenzi na matibabu wanatoa tiba mbalimbali kwa ajili ya watu wenye wasiwasi; wasiwasi ambao huwafanya wawe wanamaliza haraka sana baada ya kumwingilia mwanamke.
Kuna dawa ambayo mgonjwa akipewa zinamsaidia kurefusha muda wa kuendelea na tendo, baada ya kumwingilia mwanamke. Dawa hizo ni kama zile za kupooza msongo wa mawazo. Pia kuna mazoezi ambayo yanashauriwa kufanywa. Mazoezi haya humsaidia mtu kujenga upya mkabala wa namna anavyochukulia tendo.
Kwa wale wakazi wa Dar wanaweza kutembelea ofisi zetu za Faji zilizoko Tabata Kimanga ambapo tunatoa tiba ya tatizo hili pamoja na matatizo mengine yanayohitaji ushauri wa kisaikolojia na yale ya tiba yatilifu (Tiba mbadala).
Lakini pia njia iliyo rahisi zaidi ili kutokuwa mwepesi wa kumaliza haraka ni kujizoeza kuacha kulifikiria tendo hilo la ngono unapokaribia kufikia kileleni (kwa kufanya pole pole zaidi au kufikiria mambo mengine ya nje kama ya mpira, mfano Yanga na Simba au Manchester na Chelsea). Jenga mazoea kufanya namna hiyo. Ukizoea itakuwa ni kama kitu cha kawaida kwa kujikaza kisabuni na kuhakikisha unamsubiri mwenzio ili mwende pamoja kileleni.
Kila kitu ni kujifunza. Ukijizoeza kujikakamua bila kumaliza hata katika hali ya ham ya juu kwa kumsubiri mpenzi wako, tatizo la premature ejaculation litakuwa limethibitiwa
Mdau - Mtambuzi
0 maoni:
Post a Comment